MKUU WA MKOA WA RUVUMA AWATAKA WASIMAMIZI WA UJENZI WA MADARASA KUSIMAMIA KAZI HIYO NA FEDHA ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 29, 2021

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AWATAKA WASIMAMIZI WA UJENZI WA MADARASA KUSIMAMIA KAZI HIYO NA FEDHA ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI

 

 

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Balozi Wilbert Ibuge akizungunza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Ruanda Halmashauri ya wilaya Mbinga  ambapo amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii uku Serikali ikiendelea na mkakati wake wa kuboresha miundombinu mbalimbali ya shule, Jenerali Ibuge  alikuwa  kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali za sekondari wilayani humo.
Baadhi ya vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Ruanda wilaya Mbinga vikiwa katika hatua ya kupaua ambavyo mara ujenzi wake utakapokamilika vitasaidia kupunguza mlundikano wa wanafunzi maadarasani.

Na Muhidin Amri, Mbinga
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Balozi Wilbert Ibuge,amewaagiza wasimamizi wa miradi ya ujenzi ya vyumba vya mdarasa inayotekelezwa kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na  mapambano  dhidi ya Uvico-19 kuwa makini na matumizi ya fedha.

Balozi Ibuge alisema, ni vema kila hatua ya utekelezaji wa miradi hiyo kuwa na utaratibu wa kupiga picha ya hali halisi ili  kudhibiti udanganyifu unaoweza kufanywa na wasimamizi wasio waaminifu kwa lengo la kutafuta maslahi binafsi.

Ametoa kauli hiyo jana wakati akikagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Ruanda Halmashauri ya wilaya Mbinga vinavyojengwa kupitia fedha za mpango wa  maendeleo ya kwa Taifa na mapambano dhidi ya Uvico-19.

Alisema,ni vizuri kila hatua ya utekelezaji wa miradi ya  maendeleo sio kwa inayojengwa kupitia fedha za Uvico 19 tu,bali hata miradi mingine inayotekelezwa katika mkoa huo ipigwe picha ili  kuepuka udanganyifu unaoweza kufanywa na mafundi na wasimamizi wa miradi husika.

“kuanzia sasa nataka tubadilike katika suala zima la utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huu,nahitaji kila hatua lazima mradi upigwe picha ili kutusaidia kufahamu ubora wake na kama unalingana na thamani ya fedha zilizotolewa”alisema Balozi Ibuge.

Amewataka wataalam wa ngazi mbalimbali katika mkoa huo, kushirikiana na kusimamia kazi ya ujenzi wa miradi hiyo ili iwe na ubora na kuleta tija kama ilivyokusudiwa ya kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022 wanapata nafasi kwenye shule walizopangiwa.

Akiwa katika Halmashauri ya wilaya Mbinga,Ibuge alitembelea shule ya Sekondari Ruanda,Mkako,Shule ya Wasichana Mbinga na Kihamili kwa ajili ya kukagua  ujenzi wa miradi ya vyumba vya madarasa katika shule hizo na kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Halmashauri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mbinga Juma  Haji ameishukuru Serikali kwa kuipatia shule ya sekondari Ruanda  sh.milioni 40  ili kujenga vyumba viwili vya madarasa ambayo yanajengwa kwa mfumo wa force akaunti na  fedha zilizotumika hadi sasa ni Sh milioni 12.

Alisema, hadi sasa kazi zinazoendelea katika ujenzi huo ni kupiga ripu,kupachika grill na kuezeka na  kazi hiyo itakamilika kabla ya tarehe 10 Desemba mwaka huu.

Akiongea kwa niaba  ya Wanafunzi wenzake Miriam Komba wa kidato cha tatu,ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa uamuzi wa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Alisema, kujengwa kwa madarasa hayo kutamaliza changamoto ya upungufu wa madarasa kwa wanafunzi wa shule hiyo na hivyo kuwa na matumaini ya kufanya vizuri kitaaluma.

Hata hivyo,ameiomba Serikali kutatua changamoto kubwa ya huduma ya maji safi na salama kwani licha ya shule hiyo kuwa na miundombinu ya maji,lakini hayapatikani mara kwa mara badala yake wanalazimika kutumia maji ya mto Tip Tip ambayo sio salama kwa matumizi ya binadamu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad