HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 10, 2021

MILIONI 500 ZAREJESHA MAWASILIANO BUKOBA VIJIJINI

Na Abdullatif Yunus, KAGERA

Serikali kupitia Wakala wa Barabara Vijijini TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, imerejesha Mawasiliano ya Barabara ya Katokoro Kata Katoro, baada kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 500 kutumika katika Ukarabati wa kipande cha Barabara inayounganisha Kata za Izimbya, Mugajwale, Kyaitoke, na Ruhunga  likiwemo Daraja la Katokoro.

Barabara hiyo iliyofungwa kwa Takribani Miaka mitatu kutokana na Uharibifu Mkubwa wa Madaraja madogo madogo uliosababishwa na Mvua ambazo hunyesha Mara kwa Mara Mkoani Kagera, na kupelekea adha ya watumiaji wa Barabara hiyo hususani wakazi wa Kata Katoro na Kata jirani za Izimbya, Mugajwale, Kyaitoke, Ruhunga kushindwa kupata Huduma za msingi, sasa Mawasiliano hayo  yamerejea tena.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wananchi wa maeneo hayo wamefurahishwa na namna ambayo, shughuli hiyo imetekelezwa kwa muda mfupi na kuondoa adha waliyokuwa wakiipata, kwani eneo hilo lilikuwa halipitiki na wakati mwingine walilazimika kutumia mitumbwi jambo lililoleta usumbufu mkubwa.

Akiwa eneo hilo Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Mhe. Jasson Samson Rweikiza ameshukuru namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita imetekeleza Ukarabati huo kwa kuleta zaidi ya Milioni 500 kurekebisha eneo hilo korofi.

"...Nampongeza mkandarasi chini ya TARURA kwa kazi nzuri aliyoifanya, Barabara imeinuliwa Juu kabisa, Nina Imani hata Mvua kubwa ikinyesha hapatajaa Maji kama zamani, naishukuru Serikali kwa kutusaidia na kusikia kilio chetu.." amesema Mhe. Rweikiza.

Kurejea kwa hali hiyo katika Barabara ya Katokoro kutasaidia Wananchi kuendelea na shughuli zao za uzalishaji ikiwemo Biashara ambapo Barabara hiyo imekuwa ikitumiwa kwa kwenda minadani, pamoja na masuala ya Kijamii ikiwa ni kiungo muhimu cha kufikia Huduma za matibabu Kama Kituo cha Afya na Hospitali. 

Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt. Jasson Samson Rweikiza akizungumza Mara baada ya kufika eneo la Katokoro na kuridhishwa na Kazi iliyofanyika.

Hali ilivyokuwa eneo la Katokoro kipindi cha nyuma wakati Mvua ikinyesha na wananchi kulazimika kuvuka kwa mitumbwi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad