Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amezindua rasmi mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama DAWASA PREMIER LEAGUE.
Lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuleta hamasa na motisha miongoni mwa watumishi na kuimarisha afya ya mwili na akili.
Akizungumza
wakati wa akizindua mashindano hayo Mhandisi Luhemeja amesema michezo
hiyo itahusisha mikoa 23 ya kihuduma DAWASA pamoja na watumishi kutoka
mitambo yote ya uzalishaji maji.
Amesema
kuwa mechi ya ufunguzi zitawakutanisha watumishi wa DAWASA kutoka
Mtambo wa Ruvu Juu na Ruvu Chini, na mechi nyingine itakuwa kati ya
Watumishi wa DAWASA Makao makuu dhidi ya DAWASA Temeke mnamo tarehe 6
Novemba 2021.
Ameongeza
kuwa katika mashindano hayo zitatolewa zawadi mbalimbali kwa washindi
ikiwa ni pamoja na kombe la dhahabu, medali ya dhahabu pamoja na fedha
taslimu Tsh.200,000 kwa wafanyakazi wote wa kituo kitachoibuka mshindi
wa kwanza huku zawadi ya mshindi wa pili itakuwa medali ya Shaba pamoja
na fedha taslimu Tsh 100,000 kwa kila mfanyakazi wa kituo kilicholeta
ushindi huku mshindi wa tatu atapokea fedha taslimu Tsh. 50,000 kwa kila
mfanyakazi wa kituo kilicholeta ushindi.
Washindi
binafsi watazawadiwa Tsh.200,000 kwa mfungaji bora, Tsh.100,000 kwa
golikipa bora pamoja na Tsh. 100,000 kwa mchezaji bora.
Tamati
ya DAWASA PREMIER LEAGUE itafanyika Januari 8, 2022 katika viwanja vya
Chuo cha Sanaa na Utamaduni ADEM wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amezindua rasmi mashindano ya
mpira wa miguu yajulikanayo kama DAWASA PREMIER LEAGUE leo tarehe 1
Novemba 2021 na yatakayofikia tamati tarehe 8 Januari 2022 ambapo
fainali itafanyika kwenye viwanja vya chuo cha ADEM Bagamoyo mkoani
Pwani wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika
katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu na Utawala Bernadetha Mkandya wakiwa kwenye picha ya
pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu za DAWASA mara baada ya kuzindua
mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama DAWASA PREMIER LEAGUE leo
tarehe 1 Novemba 2021 na kufikia tamati tarehe 8 Januari 2022 wakati
wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika katika ofisi za
Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimkabidhi kombe Msimamizi wa
Mashindano Bakari Makilagi mara baada ya kuzindua rasmi mashindano ya
mpira wa miguu yajulikanayo kama DAWASA PREMIER LEAGUE leo tarehe 1
Novemba 2021 wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA
kilichofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es
Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na watumishi wa
Mamlaka hiyo wakati wa kikao cha tathmini ya utendaji kazi kwa robo ya
kwanza ya mwaka wa fedha kwa DAWASA pamoja na kuweka malengo mbalimbali.
kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mipango na Usimamizi wa DAWASA, Paul Sulley akizungumzia
kuhusu tathmini ya robo ya kwanza ya Mwaka wa fedha wa Mamlaka hiyo
wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika katika
ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimtambulisha rasmi Kaimu
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bernadetha Mkandya wakati wa
kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika katika ofisi za
Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam
Kaimu
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bernadetha Mkandya akizungumza
na wafanyakazi wa Mamlaka hivyo kuhusu namna Mamlaka ilivyojipanga
kusimamia wafanyakazi wa ngazi zote ili kuweza kuongeza ufanisi kwenye
mamlaka hiyo wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA
kilichofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya Meneja wa mikoa ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) wakifuatilia hotuba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
Salaam (DAWASA) wakifuatilia hotuba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian
Luhemeja wakati wa kikao kazi cha wafanyakazi wa DAWASA kilichofanyika
katika ofisi za Mamlaka hiyo Gerezani jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment