JJAD yashinda tuzo ya kahawa bora 2021 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 11, 2021

JJAD yashinda tuzo ya kahawa bora 2021

 Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya JJAD Kagera Farmers ( T), imeshinda tuzo ya uzalishaji bora wa kahawa nchini kwa mwaka 2021.

Mashindano hayo yameendeshwa na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), hivi karibuni wilayani Moshi Mkoa Kilimanjaro.

Kwenye mashindano hayo yaliyoshirikisha sampuli 68 za kahawa kutoka mikoa mbalimbali nchini, JJAD iliibuka kidedea kwenye kahawa aina ya Robusta kwenye nafasi ya pili na ya tatu baada ya tathmini kufanyika.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Dk. Albert Katagira amesema mashindano hayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwahamasisha wakulima kulima kahawa iliyo bora zaidi.

Amesema kwenye mashindano yaliyomalizika hivi karibuni zililetwa sampuli 68 na kisha kufanyiwa tathmini ya ubora na wataalamu wa TCB na ndipo JJAD iliibuka mshindi kwa upande wa kahawa ya robusta.

Amesema JJAD ni kampuni inayozalisha na kuuza kahawa nje ya nchi ambapo inamashamba ekari zaidi ya 100 wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Dk. Katagira amesema katika kuboresha ubotra wa kahawa, JJAD imeingia mkataba na TCB kwaajili ya kuzalisha miche bora ya kahawa ya robusta ambayo inatija kwa asilimia 100 kulinganisha na miche ya zamani.

Amesema miche hiyo bora inatokana na mbegu bora zilizotoka Shirika la Utafiti wa zao la kahawa, Tanzania Coffee Research Insitute TACRI.

Amesema miche bora ya kahawa wanayozalisha inaanza kuzalisha kahawa baada ya mwaka mmoja nanusu wakati ile ya zamani huchukua hata miaka miine kuanza kuzaaa.

Dk. Katagira amesema mche mmoja wa mbegu bora ya robusta unauwezo wa kuzalisha kilo 2.5 ya kahawa kwa mwaka wakati ile ya zamani uwezo wake ni kuzalisha nusu kilo kwa mwaka.

Amesema mipango yao kwa mwaka 2021 ni kuzalisha miche milioni 1.5 mwaka 2021-2022 miche milioni 3 mwaka 2022- 2023 miche milioni 4.5, mwaka 2023-2024 miche milioni sita na mwaka 2024- 2025 miche milioni saba.

Amesema kwa kuwa Kahawa kama kahawa inajulikana kote duniani kitu muhimu sokoni ni ubora ndiyo sababu JJAD imeamua kuzalisha kahawa yenye kukidhi ubora.

Amesema Kutokana na hilo kuanzia msimu 2019-2020, bodi ya kahawa ilianzisha mashindano ya ubora wa kahawa kwa wazalishaji wote kutoka sehemu zote nchini ili kuwafanya wakulima kuwa na utamaduni wa kuzalisha kahawa bora.

Amesema hali hiyo itasababisha kuongezeka kwa uhitaji wa kahawa kutoka Tanzania kwenye soko la dunia, pia bei ya kahawa kuongezeka kutokana na ubora unaotokana na ushindani huo, itasababisha faida kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Kampuni ya JJAD Kagera Farmers ( T), Dr Albert Katagira akionyesha vyeti ambavyo kampuni yake ilitunukiwa na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya pili na ya tatu kwa ubora wa kahawa ya robusta kwenye mashindano ya ubora wa kahawa yaliyofanyika Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya JJAD Kagera Farmers ( T), Dr Albert Katagira akiwa ameshika makombe ambayo kampuni yake ilitunukiwa kwa kushika nafasi ya pili na ya tatu katika uzalishaji wa kahawa bora aina ya robusta kwenye mashindano yaliyoendeshwa na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), hivi karibuni mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Kampuni ya JJAD Kagera Farmers ( T), Dr Albert Katagira akionyesha vyeti ambavyo kampuni yake ilitunukiwa na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya pili na ya tatu kwa ubora wa kahawa ya robusta kwenye mashindano ya ubora wa kahawa yaliyofanyika Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad