DC ILALA AWAPONGEZA VIJANA WANAOCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 2, 2021

DC ILALA AWAPONGEZA VIJANA WANAOCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI

 


Mkuu wa wilaya Ilala, Mheshimiwa Ng’wilabuzu Ndwata Ludigija, amewapongeza vijana wanaochangamkia fursa za kiuchumi ikiwamo bahati nasibu ya Biko, akisema wanaisaidia serikali kukuza pato lao badala ya kusubiri kuwezeshwa tu na kuendeleza umasikini kwa wananchi.

Mheshimiwa Ludigija ameyasema hayo wakati anamkabidhi sh milioni 10 Eugine Paullo Mbassa alizoshinda katika droo kubwa ya bahati nasibu ya Biko inayoongoza kutoa washindi wengi wakiwamo wa papo kwa hapo kuanzia sh 2500 hadi milioni 5 bila kusahau zaidi ya sh milioni 40 kila Jumapili.

“Nawapongeza vijana mnaochangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwamo kucheza Biko kwakuwa zinapunguza ukali wa maisha kwasababu isingekuwa Biko kwako wewe ina maana ingebidi uwezeshwe na mikopo ya vijana Halmashauri, lakini sasa serikali itaendelea na wengine kwakuwa wewe umeshafanikiwa kwa kupitia Biko,” Alisema dc Ludigija huku akimtaka Mbassa kuzitumia vizuri fedha za Biko.

Biko imaweza kuchezwa live kwa kuingia www.biko.co.tz pamoja na wanaotumia simu za kawaida kwa kuweka namba ya Kampuni ya 505050 na kumbukumbu 2456 huku kianzio cha kucheza kikiwa ni sh 1000 na kuendelea.

Wakati washindi wa Biko papo kwa hapo wakipatikana kila baada ya sekunde moja kwa kuchungulia nafasi kwenye gurudumua mchezo huo, wanaoshinda droo kubwa wanakabidhiwa fedha zao bank sanjali na kuwaelekeza namna bora ya kuzitumia fedha zao kwa kukuza pato lao.

Mheshimiwa Mkuu wa wilaya Ilala Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija mwenye suti akiwa katika makabidhiano ya sh milioni 10 za Biko kwa mshindi wake Eugine Paullo Mbassa katikati. Mwingine kulia ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven na kushoto ni balozi wa Biko Kajala Masanja. 

Mkuu wa Wilaya Ilala Mheshimiwa Ng’wilabuzu Ndwata Ludigija kulia akiwa na mshindi wa sh milioni 10 kutoka bahati nasibu ya Biko Eugine Paullo Mbassa katikati wakati wa makabidhiano ya fedha hizo katika tawi la bank ya NBC Viwandani jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa mshindi ni Kajala Masanja Balozi wa Biko. Picha na Mpigapicha wetu.

Mheshimiwa Mkuu wa wilaya Ilala Ng’wilabuzu Ndwata Ludigija mwenye suti akiwa katika makabidhiano ya sh milioni 10 za Biko kwa mshindi wake Eugine Paullo Mbassa katikati. Mwingine kulia ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven na kushoto ni balozi wa Biko Kajala Masanja.
 
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad