HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 22, 2021

BALOZI, JUMUIYA YA ULAYA ZAUNGA MKONO VITA DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE NA WATOTO

 




* Kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na Wasichana kwa vitendo


KATIKA kuonesha ushiriki wa kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini Balozi wa Jumuiya ya Ulaya, mabalozi, na washiriki wa kutoka Umoja wa Mataifa  wameeleza namna watakavyoshiriki katika siku 16 za uanaharakati za kupinga ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto nchini Tanzania kupitia program mbalimbali za elimu dhidi ya vitendo ikiwa ni pamoja na kujenga ueelewa zaidi kwa jamii juu matokeo ya madhara ya unyanyasaji hasa kwa wanawake na mabinti wadogo kampeni itakayoanza Novemba 25 na kuhitimishwa Desemba 08 mwaka huu Serena Hotel jijini Dar es Salaam ambapo pia kutakuwa na tamasha litakalokwenda sambamba na harambee pamoja na kuwatambua watu binafsi, taasisi na jamii kwa juhudi, ubunifu na kujitoa katika kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji.

Kampeni hiyo imehusisha Balozi za Ufaransa, Irend, Denmark, Netherlands, Ujerumani, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa wanawake kutoka Umoja wa Mataifa (UN.)

Kampeni hiyo inasisitiza kuwa unyanyasaji kwa wanawake ni uvunjaji wa haki za binadamu hivyo wanawake, wasichana na wanaume wanatakiwa kusimama imara nchi washiriki wa Umoja wa Ulaya, UNFPA na wadau mbalimbali wamejizatiti katika kukomesha vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

Akizungumza katika mkutano huo Balozi wa Jumuiya ya Ulaya Manfredo Fant amesema siku 16 za harakati za kupinga vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na Wasichana ni sehemu ya kujadili umuhimu wa kuacha vitendo hivyo, pamoja na kuwajengea  uwezo wa kujieleza waathirika ili waweze kuripoti matukio ya unyanyasaji kwa vyombo maalum.

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Nadil Hajlaoui amesema ni muhimu kuwawezesha wanawake kwa usawa hasa katika upatikanaji wa elimu na nafasi za uongozi ili kuweza kuondoa mfumo dume na kuwa na usawa katika nyanja za jamiii na uchumi na siasa.

Balozi Nadil ameishauri Tanzania kuepukana na vitendo hivyo na kutoa fursa sawa kupitia elimu na siasa na kumpongeza Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na Wasichana na kueleza kuwa Ufaransa pia kuna vitendo ashiria vya unyanyasaj kwenye siasa na elimu na ufumbuzi wa changamoto hiyo umefikia kwenye hatua kubwa.

Amesema katika kuelekea kilele shughuli mbalimbali za kijamii za kujenga uelewa kwa jamii zitafanyika ili kuhakikisha kila mmoja anatambua wajibu wake.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Jacqueline Mahon amesema vita dhidi ya ukatili wa kijinsia ni muhimu na wanaunga mkono Serikali ya awamu ya sita katika uwezeshaji wa mwanamke na Ujerumani inaipongeza Tanzania kwa jitihada na juhudi za kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia na katika mkutano wa 39 wa Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu uliofanyika Novemba 5, 2021 Tanzania ilipongezwa kwa kuandaa mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto.

Balozi wa Denmark nchini Mette Norgaard amesema ni muhimu katika kukomesha vitendo vyote vya unyanyasaji na ukatili kwa wanawake na watoto ili kujenga jamii yenye usawa na kizazi imara cha baadaye na kueleza kuwa Denmark imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania bara na Zanzibar katika kutoa elimu na kuhakikisha vitende hivyo vinakomeshwa.

Aidha Balozi wa Irish nchini Mary O'Neill amesema ni muhimu kulitambua suala hilo kwa namna linavyoathiri maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kila mmoja kwa nafasi yake kupaza sauti, kuwa wawazi na kutambua kizazi cha baadaye tunachohitaji kiwepo kwa kuwa mabadiliko yanawezeekana na kila mmoja ana nafasi katika kukomesha vitendo vya unyanyasaji.

Mwakilishi UNWOMEN Hodan Adou amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia havina kinga ila kuzuia vitendo hivyo inawezekana kwa ushirikiano wa jamii, Serikali na wadau mbalmbali na kueleza kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imejipambanua wazi kwa kupigilia msumari sheria dhidi ya vitendo vya unyanyasaji. na kuahidi kuendelea kushiriki katika harakati hizo za kupinga vitendo dhidi ya ukatili wa kijinsia ili kujenga jamii na kizazi shujaa.

Hafla ya Desemba 08 imedhaminiwa na washirika mbalimbali wakiwemo TotalEnergies, MO Foundation, Serena Hotel, Clouds Media na LALIGA itapambwa na wasanii wakubwa akiwemo Ben Paul, Nandy,  Siti and the Band, Beedja Music na Shikandito


Balozi wa Ufaransa nchini Tanzanian Nabil Hajlaoui (Kulia,) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo wa pamoja na kueleza kuwa kuelekea Desemba 08 kutakuwa na kampeni mbalimbali kwa siku 16 za kupinga  vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wasichana hasa kwa kutoa elimu ya uelewa, leo jijini Dar es Salaam. 
Balozi wa Ireland Mary O' Neill (Kulia,) akizungumza katika hafla hiyo na kueleza kuwa lazima jamii iwe ipaze sauti dhidi ya vitendo vya unyanyasaji ili kujenga jamii na kizazi shupavu, leo jijini Dar es Salaam.
Balozi waJumuiya ya Ulaya Manfreedo Fanti (watatu kushoto,) akizungumza katika mkutano huo na kueleza kuwa tamaduni ni muhimu lakini lazima kuwe na uhuru wa kujieleza bila kuwa na ugandamizi kwa wanawake na Wasichana, Leo jijini Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad