WAZIRI WA NISHATI NA NAIBU WAZIRI WAKAGUA MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE (JNHPP) - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 12, 2021

WAZIRI WA NISHATI NA NAIBU WAZIRI WAKAGUA MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE (JNHPP)

 

Waziri wa Nishati, January Makamba ( Wa kwanza kushoto), na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato ( Wa Pili kushoto)  wakiangalia mchoro unaohusu mashine za kufulia umeme (turbines) katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere. Wa kwanza kulia ni Mhandisi Mkazi wa Mradi wa Julius Nyerere, John Mageni.

UKAGUZI huo umefanyika kabla ya ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Isdory Mpango katika mradi huo itakayofanyika tarehe 12 Oktoba, 2021.

Katika ukaguzi huo, viongozi hao waliambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Felchesmi Mramba, Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila na watendaji wengine kutoka Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) na kutoka mradi wa umeme wa Julius Nyerere ( JNHPP).

Maeneo waliyokagua ni pamoja Tuta Kuu la Bwawa,  Njia za kupeleka maji kwenye mitambo ya kuzalisha umeme, Jengo la mitambo pamoja, kituo cha kupokea na kusafirisha umeme pamoja na ujenzi wa daraja la kudumu.
Waziri wa Nishati, January Makamba ( Wa Tatu kulia), akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato ( Wa Tano kushoto)  mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja la kudumu  katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere. Wa Saba kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato.  Wa Nane kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya  Nishati, Kheri Mahimbali. 
Waziri wa Nishati, January Makamba ( Wa Pili kushoto), akiangalia kazi mbalimbali zinazoendelea kufanyika  katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere. Wa kwanza kushoto ni Mhandisi Mkazi wa Mradi,  John Mageni. 
Waziri wa Nishati, January Makamba ( aliyenyoosha mkono), akizungumza jambo katika eneo inapojengwa mitambo ya kuzalisha umeme katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato.
Waziri wa Nishati, January Makamba ( Wa Nane kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na TANESCO mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja la kudumu  katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere. Wa Saba kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato.  Wa Nane kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya  Nishati, Kheri Mahimbali. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad