Vodacom Tanzania Plc yafungua duka la Vodashop Arusha ikiwa ni maadhimisho wiki ya huduma kwa wateja - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 8, 2021

Vodacom Tanzania Plc yafungua duka la Vodashop Arusha ikiwa ni maadhimisho wiki ya huduma kwa wateja

 Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Arusha Suleiman Msumi (katikati) akikata utepe kuzindua Duka la Vodashop na wiki ya huduma kwa wateja. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Vodacom Tanzania Plc Harriet Lwakatare na kulia ni Zeenat Mwindi -Meneja wa duka hilo, Vodacom Tanzania inaongeza jitihada za kuhakikisha inafikisha huduma bora kwa wateja wake kote nchini.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Arusha Suleiman Msumi akimkabidhi cheti moja ya mteja wa muda mrefu wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Plc Richard Swai kwa kutambua mchango wake baada ya kampuni hiyo kuzindua Vodashop pamoja na wiki ya huduma kwa wateja jijini Arusha leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa kampuni hiyo Harriet Lwakatare.


Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Arusha Suleiman Msumi akizungumza jijini Arusha wakati akizindua duka la Vodashop pamoja na wiki ya huduma kwa wateja leo, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc. Vodacom Tanzania Plc imezindua duka hilo ikiwa ni jitihada za kuleta huduma karibu na wateja wake nchini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad