SOKO LA BUGURUNI KUFANYIWA UKARABATI, WAFANYABIASHARA WATOLEWA WASIWASI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 8, 2021

SOKO LA BUGURUNI KUFANYIWA UKARABATI, WAFANYABIASHARA WATOLEWA WASIWASI

Soko la Buguruni upande wa wafanyabiashara wa Jumla.
Mwenyekiti wa Soko la Buguruni  jijini Dar es Salaam, Said Habibu akizungumza na Michuzi Blog leo Oktoba 08, 2021.
Mfanyabiashara wa Chakula katika soko la Buguruni, Ashura Shomi akizungumza na MICHUZI BLOG katika soko la Buguruni jijini Dar es Salaam leo Oktoba 08,2021.
Mfanyabiashara katika soko la Buguruni Vizimba B, Seil Josef akizungumza na MICHUZI BLOG katika soko la Buguruni jijini Dar es Salaam leo Oktoba 08,2021.
Mfanyabiashara wa soko la Buguruni Twalib Zubery akizungumza na MICHUZI BLOG leo Oktoba 08, 2021 katika soko la Buguruni jijini Dar es Salaam.

Eneo la Soko la Buguruni eneo la Vizimba B kwa wafanyabiashara wa Rejareja.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
MWENYEKITI wa Soko la Buguruni jijini Dar es Salaam, Said Habibu amewatoa wasiwasi wafanyabiashara wa soko hilo kuhusu sintofahamu waliyokuwa nayo.

Amewatoa wasiwasi wafanyabiashara hao mara baada ya Michuzi Tv na Michuzi blog kufika katika soko hilo leo Oktoba 08, 2021, amesema kuwa soko la buguruni lipo katika mchakato wa kufanyiwa ukarabati na ujenzi katika maeneo mawili.

Habibu amesema kuwa katika pande hizo mbili upande mmoja watajenga soko na upande mwingine watafanya ukarabati.

"Sio soko lote linaanza kujengwa kwa wakati mmoja, tunaanza na eneo la ukarabati, ukarabati huo utaanzia katika vizimba B, watu wa kuku nao wanafanyiwa ukarabati wa kawaida, mkandarasi atasakafia eneo la kuku, kubadirisha Mabati pamoja na kujenga ngazi na kuweka mabati sehemu yaliyochaka." Amesema Habibu

Amesema kuwa kwa upande wa ujenzi wa soko hilo utafanyika upande wa Machinjio, eneo la mama lishe pia watajenga upande wa Choo cha soko hilo ambacho wanatumia wafanyabiashara hao.

Maboresho hayo yamekuja mara baada ya kuona baadhi ya miundombinu hasa mitaro ya maji kujaa wakati wa mvua na kusababisha baadhi ya bidhaa kuharibika kabla hazijamfikia mlaji.

Hata hivyo Habibu amefafanua  kuwa ukarabati wa soko hilo utandelea na eneo la vizimba A.

"Kwa upande wa kuku wanawajenge Ngazi, wanapiga sakafu, wanatoa mabati yaliyoharibika na kuwawekea mabati yenye mwanga." Amesema Habibu

Licha ya hayo Habibu amesema kuwa watakarabati pia soko la wafanyabiashara wa jumla.

"Soko letu limejengwa sio kipindi kirefu sana lakini kunamakosa yalifanyika kwa upande wa wafanyabiashara wa jumla, kata zinapitisha maji kwa kiasi kikubwa  mifereji inajaa maji kwa sababu ni midogo, sakafu inajaa matope baada ya mifereji kufurika maji, wenzetu kampuni inayofadhili ukarabati huo ya Gen wameona hakuna sababu ya kuozesha matunda na kukaa katika mazingira  mabaya, kwahiyo eneo hili litafanyiwa ukarabati." Amesema Habibu

Amesema kuwa eneo la vizimba A halijajengwa tangu 1978 kwahiyo watatoa miti na mabati na watasakafia eneo lote, watajenga soko jipya la kisasa linalokwenda sambamba na uhalisia wa ukarabati.

Amesema kuwa wamekubaliana kuanza kwa awamu kwasababu wafanyabiashara wapo ndani na hawawezi kuwaondoa wote kwa kipindi kidogo ambacho ukarabati utakuwa unaendelea.

Habibu amesema kuwa wakati ukarabati unaendelea watawahamisha wafanyabiashara na kuwapa eneo jingine ili waendelee na biashara huku watakapohama wakipafanyia ukarabati na baadae watafuata wengine wanaostahili kuhama mpaka soko lote litakavyo kamilika.

"Kwahiyo  tunaanza na upande wa machinjio tumewatafutia eneo kwa kuomba eneo la mtu mwingine, pia wale wafanyabiashara wa kuku tumewapatia eneo kwa kuomba kwa majirani zetu, kwa wafanyabiashara wa vizimba B wao tumejenga mazingira ya kupewa eneo la nje ambapo kunabanda, ambapo Manispaa ya ilala watatoa mchango wao ya kufunika trubai na kuwaweka wafanyabiashara wa Vizimba B kwaajili ya kupisha mradi na hili litafanyika bila kudhurumu mfanyabiashara yeyote. " Amesema Habibu

Mwenyekiti huyo amesema atasimamia kila haki ya mfanyabiashara na arudi katika eneo lake.

"Nikiwa kama Mwenyekiti nitasimamia haki ya kila mfanyabiashara arudi katika eneo lake, hivyo kama kunahabari za kupotosha si kweli kama wanafukuzwa, si kweli kama wananyang'anywa bali ni uoga wawafanyabiashara kutokuwa na mwelekeo. 

Kwahiyo kwa kuliona hilo sisi viongozi tunaajua kuwa watu wanamikopo na wanamajukumu tumeona wabaki humu humu ili watafute liziki ya kurudisha mikopo na kupata liziki za familia zao, bado Serikali na mkurugenzi wa manispaa ya Ilala, halmashauri ya jiji la ilala, Afisa mtendaji wa kata, diwani wa kata na wakishirikiana na viongozi wa soko tunayohaki ya msingi kuwapa haki wafanyabiashara katika soko la buguruni." Amesema Habibu

Amesem kuwa wote watapata haki zako kwa mujibu wa utaratibu kwani kila mmoja anahitaji maendeleo.

Kwa upande wa mfanyabiashara katika soko la Buguruni Vizimba B, Seil Josef amesema maoni aliyoyatoa mwenyekiti wa soko la Buguruni wameyapoke na wanasubiri utekelezaji.

"Maoni aliyoyatoa Mwenyekiti wetu tumeyapokea na tupo teyari kuhama eneo hili na tunasubiri utekelezaji wa wiki tatu (3) endapo wasipotekeleza ndani ya siku hizo tutamwendea tukamuulize  vipi?....." Amesea Seil

Nae Mfanyabiashara wa soko la Buguruni Twalib Zubery amesema kuwa taarifa tumeipata kwa usahihi sasa tunasubiri utekelezaji tuu.

"Leo tumeletewa taarifa na mwenyekiti wetu kuhusu maboresho na ujenzi wa soko kwahiyo sisi tumelipokea hilo kutoka kwa uongozi wetu tunashukuru kwa hilo."

Hata hivyo Zubery ameshukuru uongozi wa soko kwa kufikiria kufanya marekebisho katika sehemu ya biashara zao ili maisha yaendelee.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad