Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayesimamia masuala ya Fedha za
Nje Bi. Amina Khamis Shaaban na Kiongozi wa Ujumbe wa Serikali ya
Ujerumani Bw. Marcus Von Essen, wakisaini Nyaraka za makubaliano ya
msaada wa Euro milioni 71 (Tsh. 190.5 bilioni) kwa ajili ya miradi
mbalimbali ya maendeleo, tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayesimamia masuala ya Fedha za
Nje Bi. Amina Khamis Shaaban na Kiongozi wa Ujumbe wa Serikali ya
Ujerumani Bw. Marcus Von Essen, wakipongezana baada ya kusaini Nyaraka
za makubaliano ya msaada wa Euro milioni 71 (Tsh. 190.5 bilioni) kwa
ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, tukio lililofanyika jijini Dar
es Salaam.

Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayesimamia masuala ya Fedha za
Nje Bi. Amina Khamis Shaaban na Kiongozi wa Ujumbe wa Serikali ya
Ujerumani Bw. Marcus Von Essen, wakionesha Nyaraka za makubaliano ya
msaada wa Euro milioni 71 (Tsh. 190.5 bilioni) kwa ajili ya miradi
mbalimbali ya maendeleo, tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayesimamia masuala ya Fedha za
Nje Bi. Amina Khamis Shaaban na Kiongozi wa Ujumbe wa Serikali ya
Ujerumani Bw. Marcus Von Essen, wakionesha Nyaraka za makubaliano ya
msaada wa Euro milioni 71 (Tsh. 190.5 bilioni) kwa ajili ya miradi
mbalimbali ya maendeleo, tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Wanaoshuhudia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Regine Hess na
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Juma Malik
Akil.

Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayesimamia masuala ya Fedha za
Nje Bi. Amina Khamis Shaaban, akihutubia baada ya kusaini Nyaraka za
ushirikiano na msaada wa Euro milioni 71 (Tsh. 190.5 bilioni) kwa ajili
ya miradi mbalimbali ya maendeleo, uliotolewa na Serikali ya Ujerumani,
Jijini Dar es Salaam.

Ujumbe
wa Tanzania na Ujerumani ulioshiriki majadiliano ya Ushirikiano kati ya
nchi hizo mbili ukimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango anayesimamia masuala ya Fedha za Nje Bi. Amina Khamis Shaaban,
wakati akihutubia baada ya kusaini Nyaraka za ushirikiano na msaada wa
Euro milioni 71 (Tsh. 190.5 bilioni) kwa ajili ya miradi mbalimbali ya
maendeleo, uliotolewa na Serikali ya Ujerumani, Jijini Dar es Salaam.

Ujumbe
wa Serikali ya Ujerumani ulioshiriki majadiliano ya Ushirikiano kati ya
nchi hizo mbili ukiwa katika picha ya pamoja na Meza Kuu. Kutoka kulia
walioketi ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Regine Hess,
Kiongozi wa Ujumbe wa Ujerumani Bw. Marcus Von Essen, Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango anayesimamia masuala ya Fedha za Nje Bi.
Amina Khamis Shaaban na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango Dkt.
Juma Malik Akil, tukio hilo limefanyika Jijini Dar es Salaam ambapo
Ujerumani imetoa msaada wa Euro milioni 71 (Tsh. 190.5 bilioni) kwa
ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ujumbe
wa Serikali za Tanzania na Ujerumani ulioshiriki majadiliano ya
Ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ukiwa katika picha ya pamoja na Meza
Kuu. Kutoka kulia walioketi ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe.
Regine Hess, Kiongozi wa Ujumbe wa Ujerumani Bw. Marcus Von Essen,
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayesimamia masuala ya
Fedha za Nje Bi. Amina Khamis Shaaban na Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akil, tukio hilo limefanyika
Jijini Dar es Salaam ambapo Ujerumani imetoa msaada wa Euro milioni 71
(Tsh. 190.5 bilioni) kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango)
*****************************
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
UJERUMANI
imeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 71, sawa na takribani
shilingi za Tanzania bilioni 190.5 kwa ajili ya kutekeleza miradi kadhaa
ikiwemo maji, uendelezaji wa maliasili na utalii, afya ya mama na mtoto
pamoja na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Nyaraka za
makubaliano ya msaada huo zimetiwa saini jijini Dar es Salaam kati ya
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayesimamia masuala ya
Fedha za Nje Bi. Amina Khamis Shaaban na Kiongozi wa Ujumbe wa Serikali
ya Ujerumani Bw. Marcus Von Essen.
Akizungumza baada ya kutiwa
saini kwa nyaraka hizo, Naibu Katibu Mkuu Bi. Amina Khamis Shaaban
aliyataja maeneo yatakayonufaika na msaada huo kuwa ni afya ya mama na
mtoto iliyotengewa Euro milioni 24 na mradi wa kuzuia migogoro baina ya
wanyamapori na binadamu, utakao tumia Euro milioni 6.
“Maeneo
mengine yatakayonufaika na fedha hizi ni mpango wa kufidia upotevu wa
makusanyo ya maduhuli katika sekta ya utalii kutokana na upungufu wa
watalii walioingia nchini kwa sababu ya ugonjwa wa UVIKO 19, kuzuia
ujangili, kuboresha miundombinu kwenye makazi na jamii inayozunguka
maeneo ya Hifadhi za Taifa, utakaogharimu Euro milioni 15” Alisema Bi.
Amina.
Alisema kuwa Euro milioni 20 zitaelekezwa kuboresha huduma
ya maji kwenye miji inayokua na kiasi kingine cha Euro milioni 3
kitatumika kuboresha usalama wa maji kwenye maeneo ya baadhi ya miji
nchini.
Bi. Amina Khamis Shaaban alisema kuwa kiasi kingine cha
Euro milioni 3 kitatumika katika masuala ya kulinda haki za akina mama
na wasichana wanaokabiliwa na changamoto ya ukatili wa kijinsia kwa
kuwapatia msaada wa kisheria.
Bi. Amina Khamis Shaaban
aliishukuru Ujerumani kwa kuanzisha majadiliano na Tanzania baada ya
kusitisha mijadala hiyo tangu mwaka 2015 na kuahidi kuwa fedha
zitakazotolewa zitatumika ipasavyo na kwa malengo yaliyokusudiwa.
Wakizungumza
katika Hafla hiyo, Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Regine Hess
na Kiongozi wa Ujumbe wa Ujerumani ulioshiriki majadiliano
yaliyofanikisha kupatikana kwa msaada huo Bw. Marcus Von Essen, walisema
Ujerumani imeamua kufufua ushiriki wake katika kujenga maendeleo ya
Tanzania ili kuunga mkono uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.
Walieleza
kuwa chini ya makubaliano mapya, Ujerumani itajikita zaidi kusaidia
afya ya mama na mtoto, kusaidia masuala ya bima ya afya kupitia NHIF,
maji na usafi wa mazingira, usimamizi wa fedha za umma, kuhifadhi maeneo
ya urithi wa dunia kama vile hifadhi ya Selous na kuwalinda wanawake na
wasichana dhidi ya vitendo vya kikatili.
Aidha, walisema kuwa
Ujerumani itarejesha mipango yake ya kusaidia miradi ya maendeleo kwa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambapo tayari nchi yao imeanza kufanya
upembuzi yakinifu wa mradi wa maji visiwani humo.
Walisema kuwa
nchi yao itatoa kiasi kingine cha fedha Alhamisi Wiki hii ambapo
mikataba ya misaada kadhaa itasainiwa kati ya nchi hiyo na Tanzania
ikiwa ni mwanzo mpya wa kuhakikisha kuwa Ujerumani inashirikiana na
Tanzania katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.
“Ninayofuraha
kwamba Tanzania inatimiza miaka 60 tangu ipate uhuru na ni muda huo huo
ambao Ujerumani na Tanzania zimekuwa katika ushirikiano ulioasisiwa na
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kiongozi wa
Ujerumani wa wakati huo Prof. Grzymek” alisema Mhe. Regine Hess, Balozi
wa Ujerumani-Tanzania.
Alibainisha kuwa Ujerumani imeongeza ahadi
zake kwa Tanzania kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka uliopita na
kwamba kutokana na hamu yake ya kutaka kuongeza zaidi misaada kwa
Serikali ya Awamu ya Sita imekuja na Msemo usemao “miradi zaidi,
ufadhili zaidi”.
Kikao hicho cha majadiliano kilihudhuriwa pia na
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil ambaye aliishukuru Ujerumani kwa kufufua
upya majadiliano kwa uamuzi wake wa kuanza kuisaidia Zanzibar katika
kutekeleza miradi yake ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment