HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 4, 2021

TARURA YAPOKEA VITENDEA KAZI VYA MAPATO KUTOKA VODACOM TANZANIA

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija akizungumza wakati wa makabidhiano hayo na kuzitaka kampuni nyingine kuiga mfano wa VODACOM Tanzania ili kujenga uchumi imara wa nchi na jamii kwa ujumla.


Mkurugenzi wa huduma za M- PESA kutoka Vodacom Epimack Mbeteni (kulia) akimkabidhi mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija (katikati) moja ya kizibao angavu kwa ajili ya vijana wanaokusanya mapato ya maegesho jijini humo, kushoto ni mhasibu mkuu wa TARURA Jacob Nyaulingo, Leo jijini Dar es Salaam.


MKUU Wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija kwa niaba ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA,)  amepokea 'Reflectors' (vizibao angavu) 400 kati ya 2000 vilivyotolewa na Kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano nchini VODACOM Tanzania vitakavyowatambulisha vijana wanaokusanya mapato ya maegesho ya magari jijini humo pamoja na kutoa elimu kwa wananchi na watumiaji wa huduma za M-PESA juu ya umuhimu wa kulipa mapato kidigitali kwa kutumia huduma ya M-PESA kwa usalama zaidi.


Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Ludigija amesema, Vodacom imekuwa kampuni ya mfano ambayo imekuwa ikishiriki shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana na serikali hasa katika kuhamasisha jamii kuhama kutoka kutumia pesa mkononi na kutumia mifumo ya kidigitali katika kulipa huduma.

Ameeleza kuwa, mafanikio ya TARURA ni jitihada za Serikali na mfumo wa kulipa gharama za maegesho kidigitali kwa kutumia M-PESA ni rahisi na salama zaidi  na kueleza kuwa serikali itaendelea kukusanya mapato kidigitali kwa usalama zaidi bila mapato kuvuja na kuwataka wananchi kutumie mfumo huo kufanya malipo ya maegesho ili kuzuia upotevu wa mapato ya Serikali pamoja na kutunza mazingira kupitia risiti za karatasi zinazotolewa baada ya kufanya malipo.

Vilevile ameipongeza Vodacom kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita hasa kwa azma yao ya kuhimiza matumizi ya huduma za fedha kidigitali na kuelimisha Umma na kuzitaka kampuni nyingine za mawasiliano kufuata nyayo za Vodacom Tanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za M-PESA Epimack Mbeteni amesema agenda ya ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kidigitali inayofanywa na TARURA ni moja ya mlengo wa kampuni hiyo ambayo ni kuhamasisha wananchi kutumia huduma za fedha kwa mifumo ya kidigitali kwa usalama zaidi, hivyo katika kushiriki katika agenda hiyo wametoa vifaa hivyo vitakavyowatambulisha vijana wanaokusanya mapato, kuwalinda pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutumia huduma za kidigitali katika kufanya malipo ya maegesho.

Mbeteni amesema vizibao angavu 400 vilivyotolewa leo ni kati ya 2000 ambavyo vitatolewa na Kampuni hiyo na kuwataka wananchi kutumia huduma hiyo ya kidigitali na kuwa malipo ya Serikali hayana tozo ya ziada na ni salama zaidi na inafaa zaidi katika kuokoa mapato ya Serikali.

Awali akitoa taarifa ya mfumo huo wa TeRMIS katika kufanya malipo mhasibu mkuu wa TARURA Jacob Nyaulingo amesema  mfumo huo ulianza kutumika Septemba Mosi, 2020 na umeleta matokeo makubwa na vifaa vilivyotolewa na Vodacom vitasaidia na kuleta hamasa zaidi kwa wananchi katika kutumia mfumo huo kwa kufanya malipo ya maegesho na hadi sasa mikoa ya Iringa, Singida, Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam wananufaika na mfumo huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad