
Na Joseph Lyimo
WANAWAKE
Mkoani Manyara, wameeleza kuwa mila kandamizi za eneo hilo zimechanjia
kusababisha wanawake kuwa na changamoto ya kutopata haki ya fursa
mbalimbali ikiwemo kutomili ardhi.
Mkoa
wa Manyara, umetajwa kuwa miongoni mwa mikoa nchini, ambayo imeendelea
kukumbatia mila kandamizi ikiwemo mfumo dume na kuwanyima wanawake fursa
ya kumiliki ardhi.
Wakizungumza
kwenye kuwapokea na kuwasalimia msafara wa kijinsia kuelekea siku ya
Mwanamke wa Kijijini, uliotokea mkoani Mwanza na kusimama Mkoani
Manyara ukielekea mkoani Kilimanjaro, baadhi ya wanawake wamepaza sauti
na kuelezea kero hiyo.
Siku
ya mwanamke wa kijijini, ambayo huadhimishwa kila mwaka mwezi Oktoba na
mwaka huu, ikibebwa na kauli mbiu ya ardhi ni nyenzo ya maendeleo kwa
mwanamke wa kijijini, pamoja na kujenga ustahimilivu kwa mwanamke
anayeishi kijijini katika kukabiliana na Uviko-19.
Mkazi
wa Kata ya Endasak Wilayani Hanang’ mkoani Manyara, Rose Gitagno
akizungumza na msafara huo ambao lengo likiwa ni kupaza sauti kwa jamii
juu ya umuhimu wa mwanamke wa kijijini kumiliki ardhi, amesema
changamoto hiyo bado ipo eneo hilo.
Gitagno
amesema miongoni mwa mikoa yenye changamoto juu ya kina mama kumiliki
ardhi ni Mkoa wa Manyara na kueleza kuwa changamoto hiyo kwa kiasi
kikubwa inachangiwa na ufinyu wa ardhi na mila na desturi zilizopitwa na
wakati.
Amesema japokuwa
mwanamke ni kiungo kikubwa cha malezi ya familia, linapokuja suala la
umiliki wa ardhi, wanaume ndiyo wanakuwa mbele na wanawake wananyimwa
hiyo haki na hata baadhi ya mila zetu, zinasema mwanamke haruhusiwi
kumiliki ardhi na ikitokea baba amefariki, watu wengine wanarithi ardhi.
Mkazi
wa Riroda Wilayani Babati, Magreth Bayo amesema elimu inapaswa kutolewa
zaidi kwa jamii ya eneo hilo ili kuelezea umuhimu wa mwanamke kumiliki
ardhi kwani mwanaume akitangulia kufa watoto na wanawake huathirika
zaidi.
Bayo amesema
endapo elimu ya usawa wa kijinsia ingetolewa kila mara na jamii
ikatambua kuwa hakuna tofauti ya mwanamke na mwanaume kwenye majukumu ya
malezi kusingekuwa na ubaguzi wa kukatazwa kumiliki ardhi.
Kiongozi
wa msafara huo, Ofisa maendeleo ya jamii wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Janeth Shishila, amesema msafara huo kutoka Mwanza umepita
mikoa mbalimbali nchini na kuelimisha jamii umuhimu wa mwanamke kumiliki
ardhi.
Amesema shughuli
kubwa za kiuchumi amekuwa akishiriki mwanamke lakini suala la matumizi
ya kupanga nani aamue nini kifanyike katika ngazi ya kaya mwanamke
amenyimwa haki hiyo.
“Tumepitia
maeneo mbalimbali na katika msafara huu, katika maeneo ambayo tumepita
tumetoa elimu ya umuhimu wa mwanamke wa kijijini kumiliki ardhi kwa
maendeleo ya familia," amesema Shishila.
Amesema
katika maeneo waliyopita, wamebaini katika mikoa mingi nchini, mila
kandamizi ukiwemo mfumo dume, umekuwa kichocheo kikubwa cha kuwanyima
wanawake fursa ya umiliki wa ardhi.
“Maeneo
mengine hawaruhusiwi kumiliki chochote katika familia na migogoro
mikubwa ya ardhi inayotokana na wanawake kunyimwa kumiliki
ardhi,"amesema Shishila.
Mwanasheria
kutoka chama cha wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) Fatuma Kimwaga,
amesema uwepo wa mfumo dume ni moja ya changamoto inayowanyima wanawake,
fursa ya kumiliki ardhi.
No comments:
Post a Comment