SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) LANOGESHA MBIO ZA CAPITAL CITY MARATHON DODOMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 11, 2021

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) LANOGESHA MBIO ZA CAPITAL CITY MARATHON DODOMA

 

MASHINDANO ya pili ya Capital City Marathon 2021, yamefanyika jijini Dodoma leo chini ya udhamini wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na kushirikisha wakimbiaji zaidi ya 2,000 kutoka kila pembe ya nchi.

Wakimbiaji kutoka Arusha na Singida waling’ara katika mbio hizo na kujinyakulia medali na vitita vya fedha taslimu.

Washindi wa mbio za 21km upande wa wanaume ni Josephati Gisemo (01:06:47)-Arusha, Hamisi Athumani (01:06:50) Singida, Yohan Sule (01:07:12) Arusha, Aloyce Simbo , Agustine Sule, Rashid Muna, Marco Joseph,  Emmanuel Gadiye, Saidi Juma na Nestory Stivin .

Washindi upande wa wanawake, Mshindi Matanga (01:20:59), Mery Naali (01:23:02), Tunu Andrea (01:23:11), Sara Ramadhani, Angel John, Ramla Phabian, Asia Dedu, Visa Mhalwa, Rose Malia na Shania John.

Washindi wa 10km wanaume ni Kaposh Laizer (29:03:16), Inyasi Sule (29:11:93) , Fabian Nelson (29:51:23), Jamali Saidi, Nelson Mbuya, Haji Luli, Elizante Elibariki, Shija Ngelela, Amani Owen na  Bosco Kangalwe.

Washindi wa 10km wanawake ni Transfora Musa (34:04:02), Anastazia Dolomogo (35:32:23), Aisha Lubuna (35:53:91), Neema Kisuda, Agnes Protas, Rebeca Bajuta, Neema Sanka, Sarah Hijti, Anna Rogath na Aisha Mohamed.

Akizungumza leo mara baada ya kukamilika kwa mbio hizo, mgeni rasmi Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema mbio hizo zimeunga mkono jitihada za serikali za katika adhma yake ya kuhakikisha inapiga vita magonjwa yasiyo ya kuambukiza .

‘’ Nashukuru kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ambaye anasisitiza wananchi kufanya mazoezi , niwaombe kila mmoja wetu akawe balozi huko tunakotoka, matukio haya yanapokuwepo mahali yanafanya mambo mengi ikiwemo lile la afya kwa sisi tuliofanya mazoezi ’’ amesema

Kwa upande wake , Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Shirika la Bima la Taifa (NIC)  Yessaya Mwakifulefule ,amesema mbio hizo ni mbio ambazo hupanda thamani kila mwaka hivyo husaidia kwa kiasi kikubwa kutengeneza ajira kwa vijana .

‘’NIC tumedhamini mbio hizi kupitia bidhaa yetu ya Bima ya Makazi  tukiwataka watanzania waweze kulinda makazi yao , hii si mara ya kwanza kwa NIC kushiriki kwenye michezo mbalimbali kwa maana ya riadha, mpira wa miguu, kwasababu tunaamini michezo ni chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana na hata serikali yetu inasisitiza kwamba vijana wajiajiri kupitia michezo’’ amesema

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Michezo Nsolo Mlozi, amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika kufanikisha mazoezi na mazoezi kwani imeweza kurahisisha maisha ya watanzania kwa kujenga undugu pamoja na urafiki’’ Leo tuko hapa watu takribani elfu mbili maana yake Dodoma imejengeka kiuchumi’’


Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson akishangilia na wakiambiaji wengine baada ya kumaliza mbilio za Kilometa 10 katika mashindano ya Riadha ya Capital City Marathon 2021 yaliyofanyika leo  Oktoba 10,2021 jijini Dodoma. Mbio za Nyika za Capital City Marathon zilidhaminiwa na Shirika la Bima la Taifa (NIC). 
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson akiakivishwa medali baada ya kumaliza mbilio za Kilometa 10 katika mashindano ya Riadha ya Capital City Marathon 2021 yaliyofanyika leo  Oktoba 10,2021 jijini Dodoma. Mbio za Nyika za Capital City Marathon zilidhaminiwa na Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Watumishi wa Shirika la Bima la Taifa wakijiandaa kukimbia 
Wakimbiaji wakiongozwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson wakijiandaa kukimbia mbio za Capital City Marathon 2021 zilizodhaminiwa na Shirika la Bima la Taifa (NIC). 
Wakimbiaji mbalimbali wakikimbia mbio hizo 
Wakimbiaji wa mbio za 5km wakijiandaa kukimbia mbio za Capital City Marathon 2021 zilizodhaminiwa na Shirika la Bima la Taifa (NIC). 


mmoja wa wakimbiaji akimaliza mbio hizo za 21KM
Wakimbiaji wakipokelewa na kuvishwa medali zao.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson akizungumza baada ya kumaliza mbio hizo ambapo alipongeza waandaaji na wadhamini wba mashindano hayo Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa kuendelea kutoa mchango wao katika michezo ikiwa ni kuunmga jitihada za Rais Samia Sulkuhu Hassan alizotaka watu washiriki michezo kwa afya na kujilinda na magonjwa mbalimbali.
Mchambuzi maarufu wa Michezo, Eddo Kumwembe nae alishiriki mbio hizo kwa kukimbia 10km.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Shirika la Bima la Taifa (NIC)  Yessaya Mwakifulefule ,amesema mbio hizo ni mbio ambazo hupanda thamani kila mwaka hivyo husaidia kwa kiasi kikubwa kutengeneza ajira kwa vijana .
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson akiakimkabidhi zawadi ya kitita cha Shilingi Milioni moja kwa mshindi za Kilometa 21 wanawake, Failuna Matanga aliyekimbia kwa Saa 1:20:59 katika Mbio za Capital City Marathon zilizofanyika leo  Oktoba 10,2021 jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Yessaya Mwakifulefule. NIC ndio wadhamini wakuu wa mbio hizo.
Washindi wakiendelea kupewa zawadi zao katika mashindano hayo. 
*************

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad