HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 27, 2021

POLISI PWANI YAWATIA MBARONI WAFUGAJI KWA KUMJERUHI MWENYEKITI CHAURU

 

Na Khadija Kalili, Kibaha

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu wawili  jamii ya wafugaji  kwa tuhuma za  kumpigia  na kumjeruhi  Mwenyekiti wa Chama Cha Umwagiliaji Mpunga (CHAURU), Ruvu Mkoani Pwani aliyetajwa kwa jina la Sadaka Chacha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani  ACP Nyigesa Wankyo kuwa Oktoba 25 saa tisa alasiri  katika mashamba yanayomilikiwa  na Chama Cha Umwagiliaji Ruvu  (CHAURU) watuhumiwa hao wakiwa  na wenzao  watatu  jumla walikua watano  walilazimisha  kuingiza  mifugo  Yao kwenye  mabwawa ya kilimo  cha Umwagiliaji  Ili mifugo yao inywe  maji.
RPC Wankyo aliwataja  watuhumiwa  hao kuwa ni Petro Ngilangu (25)na Robert Kambai (28) wote wakiwa  ni wakazi  wa Kijiji Cha Kidogozelo Kata ya Vigwaza.
Wafugaji hao walimshambulia Mwenyekit huyo wa CHAURU  Chacha kwa kumpiga  na kumjeruhi kichwani.

Tukio la kupigwa  lilitokana baada ya Mwenyekiti huyo akijaribu kuzuia mifugo kuingia ndani ya mashamba hayo, ambapo Sadala akiambatana na Daniel Mwita Ofisa pamoja na askari Mgambo walielekea eneo hilo.

Walipofika mashambani Askari Mgambo walipoona wamezidiwa walitimua mbio na kuwaacha wenzao ndipo  wakawavamia Chacha na Mwita wakawashambulia  kwa  kutumia fimbo na vitu vyenye ncha kali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad