HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 28, 2021

NAMTUMBO YAPOKEA ZAIDI YA BILIONI 1.7 UJENZI WA MADARASA

 

 

Na  Yeremias Ngerangera, Namtumbo.

Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imepokea shilingi bilioni 1,720,000,0000 kwa ajili ya ujenzi wa  madarasa katika shule za sekondari 23 na ujenzi wa madarasa katika shule shikizi za msingi 3.

Akizungumza kwenye kikao  kilichoitishwa na mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius kenneth Ningu katika ukumbi wa Halmashauri  Afisa mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Amos Kanige alisema kuwa Halmashauri imepokea fedha kiasi cha shilingi 1,720,000,000 kutoka serikali kuu  Kwa ajili ya kujenga madarasa  kwenye shule za sekondari 23 na kujenga madarasa katika shule shikizi za msingi 3.

Afisa Elimu shule za Msingi  bwana Protas Komba alisema amepokea kiasi cha shilingi  milioni120 kwa  ajili ya shule shikizi 3 zilizopata  fedha hizo   ni Mhekela,Nandengele na Ujamaa ikiwa kila shule shikiki imepewa shilingi milioni 40.

Naye afisa elimu Sekondari  Roza Nabahani kwa upande wake alidai amepokea kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kutoka serikali kuu kwa ajili ya kujenga  madarasa katika shule za sekondari 23 za Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo  Chiriku Hamisi Chilumba katika kikao hicho alimhakikishia mkuu wa wilaya kuwa shule zote zilizopata fedha kwa ajili ya kujenga madarasa yatasimamiwa kwa karibu na ofisi yake ili kuhakikisha adhima ya serikali ya kujenga madarasa iweze kutimia.

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo  kwa upande wake alidai hayupo tayari kuona ujenzi wa madarasa katika wilaya yake kujengwa kwa kiwango kisichoridhisha na kuwataka wasimamizi wa miradi hiyo kusimamia ujenzi kwa kiwango kinachotakiwa na serikali.

“ Ole kwenye hii awamu atakayebainika kushindwa kusimamia mradi katika idara yake ipasavyo na kusababisha malalamiko yasiyo  ya lazima kwa jamii katika eneo linalotekeleza mradi huo “ alisema mkuu wa wilaya huyo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wakuu wa idara na vitengo,watendaji wa kata ,makatibu tarafa,walimu wakuu na wakuu wa shule wenye miradi  na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ambapo kwa pamoja wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika kutekeleza  miradi ya ujenzi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad