HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 18, 2021

Mwendesha Mashtaka wa serikali afutiwa tuhuma za Rushwa zilizokuwa zinamkabili

 


Na John Walter-Manyara

Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara imemuondolea mashtaka ya rushwa yaliyokuwa yakimkabili Mwendesha mashtaka  wa mkoa wa Manyara Mutalemwa Kishenyi yaliyokuwa yamefunguliwa Mahakamani hapo na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoani Manyara.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Mutalemwa alipokea  rushwa ya shilingi milioni tano kutoka kwa aliyekuwa miongoni mwa wakurugenzi wa kampuni ya Mati Super Brands Ltd iliyopo mjini Babati inayozalisha pombe kali Gasper Mlay ili awasaidie katika mashtaka yaliyokuwa yanawakabili baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa yam waka 2007.

Kesi hiyo ya Jinai namba 24/2021 iliyosikilizwa kwa wiki mbili mfululizo imetolewa hukumu leo Oktoba 18,2021 kwa njia ya mtandao  na Hakimu mkazi wa mkoa wa Singida Elimo Massawe ambapo imesikilizwa Zaidi ya saa moja.

Mahakama ilidai kuwa kwenye hati ya mashtaka,Gasper  Mlay hakuwa mkurugenzi wa Mati super Brand ltd kama ilivyoelezwa kwenye hati hiyo.

Baada ya kupitia mashtaka, mahakama hiyo imejiridhisha na kuona hakuna haja ya kuendelea kumshikilia mshtakiwa kwa kuwa hakuwa na kusudio la jinai.

Upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi watano na vielelezo sita huku upande wa utetezi ukiwa na mashihidi wawili na vielelezo tisa.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Wakili wa upande wa Utetezi Lister Thadey amesema amefurahi kuona mteja wake yupo huru dhidi ya mashtaka yalikuwa yanamkabili kwa kuwa tangu mwanzo walishatambua kuwa hayakuwa na ukweli.

Mwendesha Mashtaka upande wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Manyara Martini Makani, amesema uamuzi wa mahakama unapotoka lazima upokelewe katika hali ya kawaida kwa kuwa zipo hukumu za aina mbalimbali, hivyo wanaamini haki imetendeka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad