MRADI WA MAJI MSHIKAMANO KUKAMILISHA ASILIMIA 100 ZA UPATIKANAJI WA MAJI MKOA WA DAR ES SALAAM - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 3, 2021

MRADI WA MAJI MSHIKAMANO KUKAMILISHA ASILIMIA 100 ZA UPATIKANAJI WA MAJI MKOA WA DAR ES SALAAM

 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam inatekeleza mradi wa kupeleka maji maeneo ya Mbezi Mshikamano katika Manispaa ya Ubungo mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa jitihada wa zake za kuboresha huduma katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya upatikanaji wa maji. Mradi huu utakapokamilika utakamilisha asilimia 100 za upatikanaji wa majisafi mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa utiaji wa saini ya utekelezaji wa mradi wa maji Mshikamano amesema Serikali itatoa pesa kwa ajili yabutekezaji wa mradi huo ili kuweza kuiongezea DAWASA nguvu ya kumaliza shida ya maji katika Jimbo la Kibamba ikiwemo mradi wa maji Mshikamano uliosainiwa leo.

Pia ameitaka DAWASA kusimamia miradi ya maji ili kuepuka kuhujumiwa na wananchi wasiokuwa na nia nzuri ya utakelezaji wa miradi ili kumalizika kwa wakati na kuutaka uongozi wa Wilaya ya Ubungo kuwa wakali kwenye mradi huo.

Aweso amewata DAWASA kutowabambikizia wateja wa maji bili ambazo zinakuwa kikwazo kwa wananchi na hivyo amewataka wateja wa maji kusoma Mita za maji wakiwa na wafanyakazi wa DAWASA. 

Akizungumza wakati wa kuingia mkataba na Mkandarasi Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema utekelezaji wa wa mradi huo unahusisha ulazaji wa Bomba la chuma lenye ukubwa wa kipenyo cha inchi 16 ambalo litakuwa na unbali wa Kilometa 0.35 kutoka kwenye Bomba kuu la inchi 30 linalosafirisha maji kutoka Mtambo wa Ruvu Juu hadi kwenye Kituo cha kusukumia maji eneo la Mbezi Inn.

Pia amesema katika mradi huo kutajengwa Kituo cha kupokea na kusafirisha maji ambacho ndani yake kutakuwa na tenki la kupokea maji litakalokuwa na ujazo wa Lita 540,000 pamoja na jengo la pampu ikiwemo ununuzi na ufungaji wa pampu. 

"Mradi huu utakuwa na uwezo wa kusafirisha kiasi cha Lita Milioni 23,300 za maji kwa siku ambazo zitatosheleza mahitaji ya wananchi 179,476 ambayo ni mahitaji ya miaka 20 ijayo." alisema Mhandisi Luhemeja 

Maeneo yatakayonufaika na mradi huo ni Mshikamano, Mpiji, Magohe, Msakuzi Kusini, Msakuzi Kaskazini, Machimbo, Majengo Mapya, Dodoma, Luguruni Lapaz, Mbezi Inn, Magari Saba, Magayana, Njia Panda Makondeni, TAKUKURU, Kwa Gamba, Luguruni Dampo, Luguruni KKKT, Rising Star, Msakuzi Supermarket, Aman Street, Miti Mirefu, Madafu, Kwa Mfala, Chikongowe, Masaki Street, Mbezi Msumi, Machimbo na Mageti.

Mradi huu utakanilika kwa muda wa miezi 12 na unatarajiwa kuanza mwezi Oktoba 15, 2021 na kukamilika Oktoba 2022.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akishuhudia utiaji saini wa mradi wa maji Mshikamano kati ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja(kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Advert Construction ltd Dhriv Jog(kushoto)  uliofanyika leo katika eneo la Msakuzi Center wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja(kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji  wa Advert Construction Ltd Dhriv Jog(kushoto) wakibadirishana mkataba wa utekelezaji wa wa mradi wa maji Mshikamano ukiofanyika katika eneo la Msakuzi Center wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es Salaam leo
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja(kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji  wa Advert Construction ltd Dhriv Jog(kushoto) wakionesha mkataba wa utekelezaji wa wa mradi wa maji Mshikamano ukiofanyika katika eneo la Msakuzi Center wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es Salaam leo
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akitolea maelezo kwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Mkuu wa wilaya ya Ubungo Kheri James na Mbunge wa Jimbo la Kibamba Issa Mtemvu kuhusu utakelezaji wa mradi wa maji Mshikamano wakati wa hafla ya utiaji saini wa mradi huo uliofanyika leo Ubungo Mkoani Dar es Salaam.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na uongozi wa DAWASA pamoja na wananchi wa Jimbo la Kibamba kuhusu namna Serikali ilivyojipanga kuisimamia miradi ya maji ili kuweza kuondoa kero za upatikanaji wa maji kwa wananchi ili kumtua mama ndoo kichwani wakati wa hafla iliyofanyika katika eneo la Msakuzi Center wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es Salaam leo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza kuhusu utakelezaji wa mradi wa maji Mshikamano pamoja na kutoa ufafanuzi changamoto mbalimbali zinazotokea katika majimbo 16 yanayohudumiwa na na Malmala ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) pamoja na kufikisha maji katika maeneo ya Vikindu.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba akitoa salamu za Bodi wakati wa utiliwaji saini za utekelezaji wa mradi wa Maji Mshikamano katika hafla iliyofanyika katika eneo la Msakuzi Center wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Ubungo Kheri James akizungumza kuhusu wananchi kulinda miradi wakati na baada ya kumalizika kwa miradi hiyo wakati wa utiaji saini wa mradi wa utekelezaji wa mradi wa maji Mshikamano ukiofanyika katika eneo la Msakuzi Center wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Kibamba Issa Mtemvu akizungumza kuhusu namna wananchi wa Jimbo la Kibamba walivyopata changamoto za maji  kwa zaidi ya miaka 10 na kutoa shukrani kwa DAWASA kwa kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maji hasa kumletea mameneja wambao anasaidiana nao ili kuweza kutekeleza upatikanaji wa maji katika Jimbo hilo.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akipikea maji kutoka mmoja wa wananchi waliofika  kwenye hafla utiaji saini Wa mradi wa maji Mshikamano uliyofanyika katika eneo la Msakuzi Center wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Meneja wa DAWASA, wafanyakazi wa DAWASA pamoja na wananchi wa wilaya ya Ubungo wakifuatilia utiaji saini mradi wa maji Mshikamano ukiofanyika katika eneo la Msakuzi Center wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es Salaam leo
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wakurugenzi wa DAWASA mara baada ya kumalizika kwa hafla ya utiaji saini wa mradi wa maji Mshikamano uliyofanyika leo
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa mikoa ya DAWASA mara baada ya kumalizika kwa hafla ya utiaji saini wa mradi wa maji Mshikamano uliyofanyika leo
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa kwenye picha ya pamoja na madiwani wa Manispaa ya Ubungo mara baada ya kumalizika kwa hafla ya utiaji saini wa mradi wa maji Mshikamano uliyofanyika leo
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Mkandarasi wa mradi Advert Construction Ltd mara baada ya kumalizika kwa hafla ya utiaji saini wa mradi wa maji Mshikamano uliyofanyika leo.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Ulinzi na Usalama wa wilaya ya Ubungo mara baada ya kumalizika kwa hafla ya utiaji saini wa mradi wa maji Mshikamano uliyofanyika leo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad