HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 3, 2021

EQUITY BANK YAONGEZA MASAA YA KAZI KAMA SEHEMU YA MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Benki ya Equity (T) imetangaza kuongeza muda wa kutoa huduma kwa baadhi ya matawi yake ili kuitikia mwito wa wateja wake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi la Mwenge jijini  Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Robert Kiboti amesema kuwa Benki hiyo inaendelea kuthamini uwepo wa wateja  kama sehemu muhimu zaidi ya ukuaji na ustawi wake.

"Benki ya Equity inaamini kuwa huduma bora kwa  wateja wetu ndio sehemu muhimu zaidi ya mafanikio. Sisi kwetu mteja ni familia. Ndio maana siku zote tumekuwa tukisisitiza kuwa kwetu wateja ni memba wetu, ni wadau wetu ni familia yetu. Tunapenda kutumia muda huu kusema asante kwa wateja wetu na kuwakumbusha ahadi zetu za kuendelea kuboresha huduma ili kufikia matarajio yao kwetu” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity (T), Robert Kiboti (wa pili kushoto), Mkurugeni Muendeshaji wa Benki ya Equity (T), Esther Kitoka (wa pili kulia) wakishirikiana kukata keki na mmoja wa wateja wa Benki hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuanza kwa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, iliyofanyika kwenye tawi lao la Mwenge, jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Betty Mgimba na kulia ni Meneja wa Tawi hilo, Beatrice Sanga.

Kiboti aliongeza kuwa Kutokana na maombi ya muda mrefu ya wateja wa maeneo ya Mwenge na jirani, ambao wengi wa ni wafanyabiashara na wajasiriamali,  Benki imeamua kuongeza muda wa kazi kwa tawi hilo.

“Kuanzia sasa na kuendelea, kila Jumamosi, tawi hili litafanya kazi kutoka saa tatu asubuhi mpaka saa kumi jioni, wakati kwa siku za Jumapili, tawi hili litafanya kazi kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa nane mchana” alisema Kiboti.

Kiboti pia alisema kuwa Benki itatumia wiki ya Huduma kwa Wateja kuhamasisha wateja kutumia njia mbadala za kupata huduma kama kupitia simu za mkononi yaani EazzyBanking, ATM, Huduma kwa njia ya mtandao yaani Eazzynet , na  pia kupitia Mawakala wa Benki hiyo waliopo kila kona ya nchi.

“Katika wiki hii, mimi na timu yangu tutatembelea wateja katika maeneo yao ya biashara ili kubadilishana uzoefu na kusikiliza changamoto zao. Tunataka kuwafikia katika maeneo yao  na kufanya nao mazungumzo ya ana kwa ana ili kwa pamoja tufanikiwe kufikia malengo yetu” alisema.

Kiboti alisema  pia kwamba Benki ya Equity inatarajia kufanya shughuli anuwai za kijamii wakati wa wiki hii, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika kazi za kijamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity (T), Robert Kiboti (wa pili kushoto) akimlisha kipande cha keki mmoja wa wateja wa Benki hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuanza kwa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, iliyofanyika kwenye tawi lao la Mwenge, jijini Dar es salaam leo. 

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity (T), Robert Kiboti akimsikiliza mmoja wa wateja wa Benki hiyo.

Mkurugeni Muendeshaji wa Benki ya Equity (T), Esther Kitoka akichukua risiti yake katika mashine maalumu ya kuweka fedha iliyopo kwenye tawi la Mwenge, jijini Dar es salaam.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad