Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipokea tuzo ya Mkurugenzi Mtendaji bora wa mwaka kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo katika hafla ya kutoa tuzo hizo zinazofahamika kama "The Top 100 Executive Award" iliyofanyika Oktoba 8, 2021 katika ukumbi wa Mlimani City, Da es Salaam. Benki ya CRDB pia ilishinda katika kipengele cha Afisa Mkuu Rasilimali Watu, Afisa Mkuu wa Fedha na kushika nafasi ya nne katika kipengele cha Afisa Mkuu wa Biashara. Tuzo hizo zinaratibiwa na kampuni ya EasternStar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza baada ya kutwaa tuzo ya Mkurugenzi Mtendaji bora wa mwaka katika hafla ya utoaji tuzo zinazofahamika kama "The Top 100 Executive Award" iliyofanyika
Oktoba 8, 2021 katika ukumbi wa Mlimani City, Da es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiwa na Mkewe Sekita Nsekela na Mtoto wao Amjad wakiwa ni wenye furaha baada ya kupokea tuzo hiyo.

Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Frederick Nshekanabo (katikati) akipokea tuzo ya mshindi wa kwanza katika kipengele cha Afisa Mkuu Bora wa Fedha kwa Mwaka wa 2021.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts (katikati) akipokea tuzo ya mshindi wa nne (4) wa kipengele cha Afisa Mkuu Bora wa Biashara kwa Mwaka wa 2021.Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Benki ya CRDB, Siaphoro Kishimbo akipokea tuzo ya mshindi wa kwanza katika kipengele cha Afisa Mkuu Bora wa Rasilimali watu kwa Mwaka wa 2021.
No comments:
Post a Comment