LITOLA KUMBARA KUPATA MAJI KWA MILIONI 423 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 11, 2021

LITOLA KUMBARA KUPATA MAJI KWA MILIONI 423

Mwakilishi wa Kampuni ya Tanzania Steel Pipes Ltd Emmanul
Mwambapa kulia akitiliana saini ya mkataba wa kutengeneza mabomba ya
chuma na Meneja wa Ruwasa mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshonga
katikati na meneja wa Ruwasa wilaya ya Namtumbo Davin Mkondya katikati
mkataba wa kutengeneza mabomba ya chuma kwa ajili ya mradi wa maji

Litola-Kumbara wilaya ya Namtumbo.
Meneja wa Ruwasa mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshonga kushoto na mwakilishi wa kampuni ya Tanzania Steela Pipes Ltd Emmanuel Mwambapa kulia wakibadilishana hati ya makubaliano baada ya kusaini mkataba kati ya Ruwasa na kampuni hiyo kutengeneza mabomba ya chuma yatakayotumika kukamilisha mradi wa maji wa Litola-Kumbara wilayani Namtumbo,kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya hiyo Dkt Julius Ningu.

Meneja wa wakala wa maji vijijini(Ruwasa)mkoa wa Ruvuma
Mhandisi Rbman Ganshonga akiongea jana wakati wa utiliaji saini ya
kusambaza mabomba ya chuma na kampuni ya Tanzania Steel Pipes Ltd kwa
ajili ya mradi wa maji Litola-Kumbara wilayani Namtumbo,katikati Mkuu
wa wilaya hiyo Dkt Julius Ningu.


Na Muhidin Amri, Namtumbo
WIZARA ya maji kupitia wakala wa usambazaji maji safi na salama
vijijini(Ruwasa)wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, imetenga zaidi ya Sh
milioni 423 kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Litola-Kumbara
wilayani Namtumbo.


Mradi wa maji Litola- Kumbara ulioanza kujengwa tangu mwaka 2013
unatarajia kuwanufaisha wakazi 7,927 wa vijiji viwili vya Litola na
Kumbara, ambao tangu Uhuru hawajawahi kufikiwa na maji ya Bomba hivyo
kulazimika kutumia maji yasio safi na salama katika vyanzo vya asili.


Meneja wa Ruwasa wilaya ya Namtumbo David Mkondya amesema,fedha hizo
zitatumika kwa ajili ya kununua mabomba ya chuma yatakayosambazwa
kutoka kwenye chanzo cha maji hadi kwenye tenki umbali wa km 17.76.


Mkondya amesema hayo jana,baada ya kusaini mkataba na Kampuni ya
Tanzania Steel Pipes Limited kwa ajili ya kutengeneza mabomba ya
chuma yatakayotumika kusambaza na kufikisha maji.


Amesema, mradi wa maji Litola- Kumbara ulisainiwa mwezi Oktoba mwaka
2013 na utekelezaji wake ulianza mwaka Januari 2017 na ulitarajiwa
kukamilika Desemba mwaka 2019 chini ya Mkandarasi Vibe International
Company Limited ambayo ilishindwa kukamilisha kazi hiyo.


Kwa mujibu wa Mkondya, mradi huo unakamilishwa na Ruwasa kwa njia ya
force Akaunti na hadi sasa kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa matenki
mawili yenye ujazo wa lita 100,000 na lita 75,000,ujenzi wa chanzo cha
kukusanya maji na uchimbaji mtaro na kulaza mabomba ya kusambaza maji
umbali wa km 22.


Amesema, kazi nyingine zilizotekelezwa ni kuchimba mtaro na kulaza
bomba kuu kutoka katika chanzo umbali wa km11 kati ya km 17.76,ujenzi
wa vituo 32 vya kuchotea maji na kujenga mifumo ya mfano ya uvunaji wa
maji ya mvua.


Naye Meneja wa Ruwasa mkoa wa Ruvuma Rebman Gansonga amesema, katika
kutatua kero ya maji kwa wananchi wa vijiji hivyo na maeneo mengine ya
mkoa wa Ruvuma,Ruwasa inashirikiana na viongozi wa Serikali kuanzia
ngazi ya vijiji,kata,wilaya na mkoa.


Amesema,mradi wa maji Litola-Kumbara umeshindwa kukamilika kwa wakati
kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mkandarasi wa awali
kushindwa kutekeleza kazi hiyo na hivyo wizara ya maji kulazimika
kuvunja mkataba wake.


Gansonga amesema, baada ya kupata bomba za chuma kazi hiyo
itakamilika nah DI kufikia mwezi Februari mwakani maji yataanza
kupatikana na wakazi wa vijiji hivyo kufikiwa na huduma ya maji safi
na salama.


Amesema,wameamua kusaini mkataba huo katika eneo la mradi ili wananchi
ambao ni wanufaika wa mradi huo waweze kushuhudia na kurudisha
matumaini yaliyotoweka hasa kwa kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa
muda mrefu bila mafanikio.


Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Ningu amewaka wananchi
kuhakikisha wanatunza mradi na miundimbinu yake ili uweze kudumu na
kuharakisha maendeleo.


Aidha Dkt Ningu,ametaka utekelezaji wa miradi yote ya maji
inayofanyika katika wilaya hiyo ofisi yake ifahamishwe badala ya
kufanywa kinyemela ili waweze kuifahamu na kufuatilia utekelezaji
wake.


“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria sana kumtua Mama ndoo
kichwani, lengo ni kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inawafia
wananchi karibu na kuwaondolea usumbufu wa kutembea umbali mrefu,kwa
hiyo ni vyema miradi hiyo ifahamike”amesema Dkt Dc Ningu.


Naye mwakilishi wa kampuni ya Tanzania Steel Pipes Limited Emmanuel
Mwambapa, amehaidi kuzalisha mabomba kwa wakati na yenye viwango ili
kukamilisha mradi huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi wa
vijiji vya Litoka na Kumbara.


Ameziomba mamlaka za maji hapa nchini,kutumia mabomba yanayozalishwa
na kamapuni hiyo kwenye ujenzi wa miradi ya maji kwa kuwa ni bora na
imara,badala ya kununua mabomba na vifaa vinavyozalishwa na viwanda
vya nje.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad