HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 18, 2021

KUFUNGWA KWA LAINI MILIONI 2.9, UVIKO-19 KWASABABISHA HASARA VODACOM



* Yajizatiti kulipa wanahisa wa Kampuni hiyo


KAMPUNI Ya Teknolojia ya Mawasiliano nchini Vodacom PLC imesema kuwa kufungiwa kwa laini zisizosajiliwa kwa alama za vidole milioni 2.9 zilizokuwa zikitumiwa na wateja wao na janga la UVIKO-19 vimeisababishia kampuni hiyo hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 30 hali iliyopelekea kampuni hiyo kushindwa kuwalipa wanahisa mwaka 2020.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Vodacom PLC Jaji mstaafu Thomas Mihayo mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kwa waandishi habari juu ya kikao cha 5 cha wanahisa wa kampuni hiyo na kueleza kuwa kampuni hiyo haikuweza kulipa salio kwa wanahisa mwaka uliopita kutokana na ugumu wa biashara uliosababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO- 19 pamoja na kufutwa kwa wateja milioni 2.9 waliokuwa wanatumia mtandao huo hali iliyosababisha ugumu wa biashara na uendashaji kampuni hiyo hasa katika kufanya matengenezo ya mikonga nchi nzima.

Jaji Mihayo amesema, katika mkutano huo takribani wanahisa 2260 walishiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao na kujadiliana na kufikia muafaka wa matumaini ya kulipa salio kwa wanahisa wao.

Aidha amesema katika mkutano huo wametoka na maazimio 14 ambayo yamepitishwa ikiwemo kuondoka kwa Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Hisham Hendi ambaye amepata kazi nyingine ya kuitumikia na bodi hiyo kuridhia na mchakato wa makabidhiano na mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo Sitholizwe Mdlalose unaendelea baada ya kukubaliwa na wanahisa.

Kuhusiana na suala la tozo katika miamala ya simu Jaji Mihayo amesema, suala la tozo limetikisa biashara kutokana na wateja wengi walikuwa wanatumia njia za mtandao kutuma na kupokea fedha na licha ya mabadiliko bado hali haijatulia.

Kwa upande wake Mkurugenzi anayemaliza muda wake ameishukuru Serikali kwa ushirikiano alioupata pamoja na timu ya Vodacom na bodi ya wakurugenzi kwa ushirikiano uliotuka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad