HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 18, 2021

HALI YA LISHE NCHINI YAIMARIKA, KILELE CHA LISHE KUFANYIKA OKTOBA 23 MKOANI TABORA,

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dkt. Germana Leyna akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 18,2021 na kutambulisha Kilele cha maadhimisho ya siku ya lishe Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Tabora katika viwanja vya Nane nane Ipuli Mkoani Tabora Oktoba 23, 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dkt. Germana Leyna akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 18,2021.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
TAKWIMU zinaonesha kuwa hali ya lishe nchini inazidi kuimarika kutokana na kupungua kwa viwango vya utapiamlo hapa nchini kwani udumavu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano vimepungua.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dkt. Germana Leyna wakati akitambulisha Kilele cha maadhimisho ya siku ya lishe Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Tabora katika viwanja vya Nane nane Ipuli Mkoani Tabora Oktoba 23, 2021.

Akizungumza leo Oktoba 18, 2021 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kiwango cha Udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kimepungua kutoka asilimia 34.7 kwa mwaka 2014 hadi asilimia 31.8 kwa mwaka 2018.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO 1995) licha ya kupungua kwa viwango vya utapiamlo lakini shirika hilo linaonesha kuwa hali ya lishe bado ni mbaya kwani inakadiliwa kuwa kunawatoto zaidi ya milioni tatu wamedumaa.

Dkt. Germana amesema kuwa idadi kubwa ya watoto wenye udumavu wapo katika mikoa 11 hapa nchini ambayo ni Dar es Salaam, Kagera, Kigoma, Mara, Dodoma, Geita, Tanga , Ruvuma, Mbeya, Morogoro na Tabora.

"Mikoa inayoongoza kwa utapiamlo ni mikoa inayozalisha mazao ya chakula na kufanyabiashara, sio kuweka mezani na kula, hivyo nishauri jamii kuzalisha mazao na kuweka mezani sio kufanyia biashara tu." Amesema Dkt. Germana

Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya Lishe hapa nchini ni " Lishe bora ni Kinga Thabiti dhidi ya magonjwa; Kula mlo Kamili, fanya Mazoezi, kazi iendelee."

Maadhimisho ya kitaifa mwaka huu 2021 mkoani Tabora yana lengo la kuwaweka pamoja wadau wa lishe, ambao ni viongozi, wanasiasa, wataalamu, wadau wa maendeleo, Mashirika yasiyo ya kiserikali na wananchi ili kuongeza ufahamu kuhusu umhimu wa lishe kama msingi wa afya bora na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Dkt. Germana amesema kuwa Maadhimisho ya mwaka huu yatatanguliwa na shughuli mbalimbali za afya na lishe kuanzia Oktoba 18, 2021 hadi Oktoba 22, 2021, moja ya shughuli hizo ni kufanya maonesho ya bodhaa na vyakula vilivyoo gezwa virutubishi kutoka sambani au kiwandani.

Dkt. Germana amesema kuwa viwango vya ukondefu kimepungua kutoka alisimia 3.8 kwa mwaka 2014 hadi kufuikia asilimia 3.5 kwa mwaka 2018. pamoja na kupungua kiwango hicho lakini  bado kuna watoto laki sita wanautapiamlo mkali na wakadiri. Huku tatizo la uzito pungufu likiwa limeongezeka kutoka asilimia 13.4 kwa mwaka 2014 hadi asilimia 14.6 kwa mwaka 2018.

Aidha Dkt. Germana watu wazima tatizo la upungufu wa damu miongoni mwa wanawake walio katika umri wa kuzaa wa miaka 15 hadi 49 limepungua kutoka asilimia 44.8  hadi asilimia 28.8.

"Tatizo la uzito uliokithiri kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa limeongezeka kutoka asilimia 29.7 kwa 2014 hadi 31.7 kwa takwimu za 2018, uzito uliozidi na kiribatumbo ni chazo kikuu cha magonjwa sugu yasiyoambukiza yanayosababishwa na ulaji duni na mtindo mbaya wa maisha magonjwa hayo kama kisukari, figo, moyo na baadhi ya Saratani."Amefafanua Dkt. Germana

Dkt. Germana amesema  kuwa lishe bora huimarisha kinga ya mwili na hivyo husaidia kupunguza ukali wa maradhi pamoja na vifo vitokanavyo magonjwa ya kuambukiza ikiwemo UVIKO 19.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad