WATOTO WASIHUSISHWE KWENYE MIGOGORO YA KIFAMILIA KWANI INASHUSHA TAALUMA ZAO- MFINANGA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 12, 2021

WATOTO WASIHUSISHWE KWENYE MIGOGORO YA KIFAMILIA KWANI INASHUSHA TAALUMA ZAO- MFINANGA

 

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

WAZAZI na walezi ,wameaswa kuacha kuhusisha watoto kwenye migogoro ya kifamilia pale inapotokea, kwani watoto hao bado hawana uwezo wa kubeba mambo ya kifamilia na masomo kwa wakati mmoja ,hali inayosababisha kuyumba kitaaluma.

Pia wametakiwa ,kupunguza ubize na kufuata majukumu yao ya malezi ikiwa Ni pamoja na kuwafuatilia muenendo wa masomo yao.

Rai hiyo ,ilitolewa na meneja wa shule za Kibaha Independent (KIPS) pamoja na Kibaha Annex , Nuru Mfinanga ,wakati wa mahafali ya 16 KIPS na Annex ikiwa ni mahafali ya kwanza ya kuwaaga wahitimu wa darasa la saba mwaka 2021 wapatao 107.

Nuru alisema ,kwa kuhusisha mambo ya migogoro ya kifamilia majumbani inawaharibu watoto kisaikolojia.

"Tunachanganya watoto kisaikolojia, mwanafunzi akiwa darasani anakuwa  na mawazo yaani hayupo darasani kabisa ,na ukimfuatilia mtoto wa aina hii lazima utakuta hafanyi vizuri kimasomo"alisisitiza Nuru.

Mwenyekiti wa shule hizo, alhaj Yusuph Mfinanga, ameeendelea kutoa kilio chake Cha kuanzisha sekondari japo kuwa nia hiyo imekuwa ikikabiliwa na vipingamizi mbalimbali .

Alisema ,walishanunua shule ya Pwani sekondari kupitia mnada wa mahakama na matarajio ni kuigeza kuwa KIPS sekondari lakini kukatokea vizuizi kwa takriban miaka mitatu sasa.

"Tumekaa vikao ,tumeona fedha yetu tuliyonunulia hairudishwi ,na shule hiyo wameinunua ikiwa haina hati hivyo wameamua kuendelea na mchakato wa vibali vya kujenga na usajili ili mwakani shule ianze kutoa elimu "alisisitiza Mfinanga.

Awali mzazi , Abubakari Alawi alieleza, serikali ya awamu ya sita inajitahidi kuboresha mazingira bora ya elimu ,Anatoa wito kwa halmashauri kuanza maandalizi ya miundombinu mapema ili wanafunzi zaidi ya milioni moja 2021,wanaotarajia kuingia kidato cha kwanza mwakani waingie darasani .

"Sio inafikia muda wa kuingia kidato cha kwanza ndio halmashauri zinakimbizana kuchimba msingi wa ujenzi ,lakini naimani serikali ipo imara kwa kuwajengea mazingira mazuri watarajiwa":;'aliongeza Alawi.

Nae mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri akiwakilishwa taarifa yake na ofisa tawala wilaya ,Asia Mwinyihaji alisema elimu waliyoipata wahitimu hao ,ikafungue milango ya maisha yao.

Aliwahakikishia wamiliki wa shule hiyo ,kuwapa ushirikiano katika changamoto zitakazowakabili.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad