UPANA WA MTANDAO WA VODACOM TANZANIA – KIUNGANISHO MUHIMU MAENEO YA VIJIJINI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 26, 2021

UPANA WA MTANDAO WA VODACOM TANZANIA – KIUNGANISHO MUHIMU MAENEO YA VIJIJINI

 

 

 

Teknolojia pamoja na uunganishwaji vina uwezo mkubwa hujenga jamii yenye usawa na ushirikishwaji zaidi. Upatikanaji wa mtandao wa intaneti ni kitu kinachowezesha ushiriki kiuchumi. Hii ni sababu kuu ya kwa nini Vodacom Tanzania, ikiwa inaongoza katika soko la mawasiliano ya simu, imeweka kipaumbele kwenye upatikanaji wa mtandao wa mawasiliano kwa jamii za vijijini ambazo hazijawahi kuwa na mawasiliano hayo kupitia mpango wake wa kuongeza kasi ya uunganishaji maeneo ya vijijini.

Ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa ‘Africa.connected ambao unaendana na mpangokazi wake ujulikanao kama Mkataba wa Jamii kuhakikisha utumiaji mpana wa mtandao wa intaneti miongoni mwa Watanzania. Vodacom imejiwekea lengo la kufikisha uunganishwaji wa mtandao kwa kasi ya broadband kwa asilimia 65 ya wananchi ifikapo mwishoni  mwa mwaka 2021 na lengo la mwisho ni kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2024.

Hatua hii pia inaendana na lengo la serikali lililotangazwa la kuongeza uunganishwaji wa mtandao wa broadband kutoka asilimia 45 hadi kufikia asilimia 80. Hadi sasa, eneo lililounganishwa na Vodacom linawafikia asilimia 52 ya wakazi walio katika vijiji 1,184 nchini.

Kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), Vodacom imepanua eneo la mtandao wake katika maeneo ya vijijni kuweza kuwafikia asilimia 92 ya wananchi, na hivyo kujihakikishia nafasi yake ya uongozi katika utoaji wa huduma za mawasiliano, ikitoa huduma bora zaidi za sauti na data pamoja na huduma nyingine za kifedha na kijamii.

Kwa zaidi ya miaka 20, Kampuni ya Vodacom imekuwa ikiendelea kuwekeza na kuboresha mtandao wake ili kuhakikisha kuwa inatoa huduma bora kabisa kwa wateja wake na kuwapatia teknolojia mpya na bidhaa za ubunifu wa hali ya juu kuliko zingine zinazopatikana sokoni. Kutokana na uwekezaji huo, ambao una thamani ya zaidi ya Shilingi 171.4 bilioni, kwenye teknolojia ya 4G peke yake, Vodacom ina minara zaidi ya 3,000 yenye uwezo wa 2G, zaidi ya 2,800 ya 3G na zaidi ya minara 2,000 ya 4G, ikiwa na mtandao mpana kuliko yote nchini na ambao unawafikia wananchi asilimia 92.

Mkakati na sera za serikali ni zaidi ya kuwa na mtandao mpana tu bali pia inahitaji kuhakikisha kuwa upatikanaji wa huduma hiyo ni wa haki na usawa kwa watu wake. Kwa kufanya kazi na vyombo mbali mbali vya serikali na mashirika binafsi, Vodacom inachangia mpango huu wa serikali kwa kuleta simu za bei nafuu sokoni, kwa kuwapa watumiaji huduma zenye tija kwa mahitaji yao kwa wale wenye matatizo ya kusikia au kuona pamoja na kutoa misaada ya moja kwa moja kwenye shughuli nyingine za serikali.

Mtandao huu ambao msingi wake ni teknolojia za kisasa kabisa na huduma na bidhaa zinazohitajika, unawapa watumiaji wa Vodacom fursa ya kufaidika kutokana uunganishwaji huo. Huduma mojawapo ni M-Pesa ambayo imejipatia watumiaji zaidi ya milioni 10 nchi nzima ikiwa na mtandao wa mawakala zaidi ya 107,000. Mfumo huu umekuwa na kuweza kuwafikia watumiaji wa vijijini ambao bila hivyo wangekosa huduma rasmi za kifedha.

Vile vile, mfumo huu pia ni msingi wa kuunganisha wakulima kupata taarifa muhimu pamoja na kufanya malipo yao kupitia huduma ya M-Kulima, ambayo ina watumiaji zaidi ya 10,000.

Takwimu zilizopo zinathibitisha kuwa Vodacom ina mtandao mpana kuliko mingine nchini, wenye kasi kubwa zaidi ya 4G na idadi kubwa zaidi ya watumiaji. Kupitia kampeni yake ijulikanayo kwa jina la “Kimbiza na 4G ya Ukweli”, Vodacom inasisitiza kuwa mtandao hauna maana tu ya upana bali pia ubora ni muhimu. Utafiti huru umeonesha kuwa mtandao wa Vodacom unaongoza na hivyo kuwaacha nyuma washindani wake kwenye maswala ya kasi, uimara na tija.

Kutokana na teknolojia yake bora kuzidi ile ya washindani wake, Vodacom Tanzania Plc, inaweza kutumia mtandao wake kutoa huduma muhimu na uunganishwaji wa uhakika ukiwa na mfumo rafiki kwa watumiaji wake, hivyo kuwezesha Watanzania wengi zaidi kufaidi Maisha ya kidijitali.

Mpango huu umefikisha kampuni kuwa na mtandao imara zaidi wa 4G na mpana kuliko mingine nchini, unaoendeshwa kwa kasi ya 27mbps ambayo ni kasi mara mbili ya mshindani wake wa karibu. Uwezo huu mkubwa kiufundi na upana wa mtandao una maana kuwa watumiaji wa Vodacom wanapata kuunganishwa kwa namna ya kipekee kwenye mtandao wa intaneti, pamoja na huduma bora za sauti na ujumbe mfupi.

Upana wa mtandao wa Vodacom, unaofikia maeneo yote ya nchi pia ni msingi wa utoaji wa huduma zinazookoa maisha kwa watumiaji walioko vijijini. Kwa ushrikiano na hospitali ya CCBRT kwa mfano, zaidi ya wagonjwa 6,000 wa fistula wamepata huduma za upasuaji, wengi wao wakiwa wametokea vijijini.

Kuna faida nyingi zaidi zitokanazo na kuunganishwa kwenye mtandao wa mawasiliano. Mtandao mpana unawapa wadau mbalimbali, washirika na wabunifu fursa anuai za kuandaa na kufikisha bidhaa na hivyo kujenga jamii yetu na taifa kwa ujumla kijamii na kiuchumi. Huduma hizi ni pamoja na elimu, afya, biashara na hata burudani.

Katika kuelekea kwenye Jamii ya Kidijitali, Vodacom Tanzania Plc imejenga mtandao wa data wa kitaifa wenye kasi na wenye kuaminika unaowapatia watumiaji wote huduma za intaneti kwa bei nafuu, kuongeza ushirikishwaji kwa jamii zilizotengwa na hata kusaidia kupunguza makali yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa. Yote haya, ikiwa vilevile ni kampuni inayoongoza kwa kiwango kikubwa cha ulipaji kodi katika sekta nzima ya mawasiliano, ambapo katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020 ililipa Shilingi trilioni 1.9 ikiwa ni kodi kwa serikali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad