HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 30, 2021

SERIKALI YAPELEKA VIFAA TIBA HOSPITALI YA CHALINZE, RIDHIWANI KIKWETE ASHUKURU

 

Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
 

SERIKALI  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanoa leo imetimiza ahadi zake zilizotolewa na Rais wa Samiah Suluhu Hassan kwa kupeleka vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani.

Vifaa hivyo vina thamani ya Shilingi Milioni 480 ikiwemo mashine ya Kupiga picha za Mionzi yaani X-Ray, Jokofu la kuhifadhia maiti, mashine za kupimia damu na vifaa mbalimbali.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kwa vifaa hivyo Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameishukuru Serikali kwa kutekeleza ahadi hii ndani ya muda wa wiki tatu toka kutolewa kwa ahadi.

Wananchi wa Kata hiyo wakiongozwa na wakina mama ambao walikuwa ipokea wameshangilia na huku wazee wakimuombea Mungu amlinde Rais wa nchi yetu.




 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad