NEMC YAWASILI MKOANI TABORA ILI KUFANYA UKAGUZI KATIKA MGODI WA DHAHABU WA KITUNDA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 23, 2021

NEMC YAWASILI MKOANI TABORA ILI KUFANYA UKAGUZI KATIKA MGODI WA DHAHABU WA KITUNDA

 

NA TIGANYA VINCENT

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) limewasili Mkoani Tabora kwa ajili ya ukaguzi wa Mgodi wa uchimbaji dhahabu uliopo Kitunda wilayani Sikonge.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Dkt. Samwel Gwamaka baada ya kusaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Alisema wanakwenda kuangalia kama shughuli za uchimbaji  zinazingatia taratibu uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwenye eneo hilo.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani alikuwa na ziara katika eneo hilo na kukuta makazi ndani ya eneo la mgodi  hali ilimlazimisha kutoa amri ya kuondoa makazi na watoto walionekana katika eneo hilo.

Aliagiza ndani ya mgodi huo wabaki wachimbaji pekee yao na familia zilizomo humo zielekee Kijiji Kitunda kwa ajili ya usalama wao na watoto wao.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(kushoto) akiwa katika picha ya pamoja leo na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Dkt. Samwel Gwamaka (kulia) .Mkurugenzi Mkuu huyo wa NEMC alipita Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa akiwa  njiani kuelekea katika ukaguzi wa Mgodi wa Uchimbaji madini ya dhahabu wa Kitunda wilayani Sikonge.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(kushoto) akimkabidhi leo zawadi ya asali ya Tabora  Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Dkt. Samwel Gwamaka (kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(kushoto) akimuonyesha asali iliyofungashwa vizuri Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Dkt. Samwel Gwamaka (kulia) . Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Dkt.  Gwamaka aliwasili Tabora kwa ziara ya ukaguzi wa Mgodi wa dhahabu wa Kitunda.

Picha na Tiganya Vincent

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad