Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akifungua
Kongamano la Wadau wa Kitaifa kuhusu upatikanaji wa Rasilimali za kusaidia
utekelezaji wa Mikakati ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Kongamano hilo limefanyika hii leo 23/09/2021 katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma. Wengine katika
picha ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba, Balozi wa Uingereza nchini
Mhe. David Concar na Mkurugenzi wa REPOA Dkt. Donald Mmari.Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar akihutubia wadau
walioshiriki kongamano la Kitaifa kuhusu upatikanaji wa Rasilimali za kusaidia
utekelezaji wa Mikakati ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Mhe. Balozi amesisitiza kuendelea kushirikiana na Tanzania katika jitihada za
kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiteta
jambo na Mkurugenzi wa REPOA Dkt. Donald Mmari (kushoto) mara baada ya kufungua
Kongamano la Wadau wa Kitaifa kuhusu upatikanaji wa Rasilimali za kusaidia
utekelezaji wa Mikakati ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi hii leo katika ukumbi wa Royal Village Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew
Komba.Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar akizungumza na Bw.
Richard Muyungi ambaye ni Mjumbe wa Green
Climate Fund kwa niaba ya Afrika, kuhusu Maandalizi ya Mkutano wa Glasgow
hasa matarajio ya Afrika na Tanzania katika Mkutano huo kuhusu upatikanaji wa
fedha za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
No comments:
Post a Comment