HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 22, 2021

Naibu waziri wa Sanaa,Utamaduni na Michezo atangaza Neema wana Michezo Babati

 

Na John Walter-Manyara

Mbunge wa Jimbo la Babati mjini (CCM), ambaye pia ni Naibu waziri wa Sanaa,Utamaduni na Michezo Pauline Gekul, anatarajia kuanzisha  mashindano ya Michezo mbalimbali yenye jina Gekul Cup 2021, yatakayoshirikisha kata zote nane za jimbo hilo kuanzia Oktoba 1 mwaka huu.

Akizungumzia mashindano hayo akiwa ofisi ya Jimbo mjini Babati leo Septemba 22,2021 Gekul alisema lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji, kutoa fursa za ajira kwa vijana pamoja na kuleta mshikamano katika jamii yakiongozwa na kauli mbiu isemayo “Kipaji ni Uchumi”.

 Gekul alisema kwa sasa hakuna sekta inayofanya vizuri katika kutoa ajira kwa vijana kama michezo huku akisistiza umuhimu wa kushiriki michezo kwa lengo la kuhamasisha Amani na kuimarisha afya.

Gekul amesema Mashindano hayo yatakuwa katika michezo ya Mpira wa Miguu kwa wanaume na wanawake,mpira wa pete na Riadha ambapo itafanyika katika ngazi ya kata kwenye kata zote na mitaa yake na washindi watakutanishwa kwenye mchujo na kupata mshindi wa jimbo.

Naye mjumbe wa kamati ya Gekul cup 2021 ambaye pia ni kiongozi wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Babati (BDFA) Mwalimu Dennis Bakuza alisema maandalizi yanaendelea vizuri.

Kuhusu Zawadi zitakazotolewa kwa washindi Bakuza amesema zitatangazwa baadaye.

Kata zitakazoshiriki mashindano hayo ni Maisaka, Bagara,Sigino,Mutuka,Nangara,Singe,Bonga na Babati.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad