NAIBU WAZIRI MWANAIDI ALI KHAMIS AFANYA ZIARA WILAYANI BIHARAMULO MKOANI KAGERA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 17, 2021

NAIBU WAZIRI MWANAIDI ALI KHAMIS AFANYA ZIARA WILAYANI BIHARAMULO MKOANI KAGERA


Uongozi wa Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera umetakiwa kuweka mifumo madhubuti ya usimamizi wa miradi mbalimbali inayojengwa na Serikali kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha inayotumika katika ujenzi wa miundombinu hiyo.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis katika ziara yake kwenye zahanati ya Kaniha, Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera ikiwa ni sehemu ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Mhe. Mwanaidi pia amewataka wananchi wa Kata ya Kaniha kuhakikisha wanakuwa walinzi wa miundombinu inayojengwa kwa lengo la kuwaondolea changamoto zinazotokana na huduma duni.

Amesema miradi mbalimbali inajengwa kwa kutumia nguvu na rasilimali za taifa ikiwemo michango ya wananchi hivyo, Serikali kupitia maeneo husika inatakiwa kuweka mifumo sahihi ili kuwawezesha wananchi kupata huduma bora za jamii.

“Niwatake wananchi wa kata hii kuwa walinzi wa miundombinu hii ili iweze kuwahudumia kama ilivyokusudiwa”.

Ameongeza kuwa Serikali inakusudia kuwawezesha wananchi kupata huduma bora na hiyo ni moja ya vipaumbele vya Serikali ya awamu ya sita ambayo inaweka mkakati wa kuboresha huduma za uzazi, mama na mtoto.

Akiwa katika eneo hilo, Mhe. Mwanaidi alishiriki kuamsha ya ari ya kujiletea maendeleo kwa kuchanganya na kumwaga zege katika ujenzi wa zahanati ya Kaniha na baadaye kuuunga mkono juhudi zao kwa kuchangia mifuko 50 ya saruji ikiwa ni katika ujenzi wa zahanati hiyo.

Akisoma risala ya Kata, Mwalimu Emily Kabote amesema wananchi kilichowasukuma wananchi kuamua kuanizsha ujenzi wa zahanati hiyo ni kuongezeka kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hadi watu 11572 kwa mwaka hivyo uongozi wa kijiji kwa kushirikiana na wananchi waliamu kuanzisha ujenzi wa majengo mengine ulianza mwkaa 2014.

Amesema hadi sasa ujenzi huo umegharimu kiasi cha shilling millioni 94 na vyuma sita vimekamilika na vinafanya kazi pamoja na juhudi za wananchi kujiletea maendeleo sambamba na kuchangia nguvu zao katika maendeleo bado wananchi wanahitaji kuungwa mkono katika juhudi hizo kutoka kwa Serikali na wadau .

Naibu Waziri anaendelea na ziara yake Mkoani Kagera kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na huduma za jamii kwa makundi maalum ya watoto, wanawake na Wazee.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Mwenye kiremba) akisaidiana na Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Kemilembe Lwota kumwaga zege katika Ujenzi wa Zahanati ya Kaniha Wilayani Biharamulo ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji jamii kuchangia nguvu zao katika miradi mbalimbali ya maendeleo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Mwenye kiremba) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Kemilembe Lwota (kulia) wakishiriki katika kuchangia nguvu zao katika miradi ya maendeleo kwa kuchanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kaniha, Wilayani Biharamulo, Kagera.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Mwenye kiremba) akikabidhi mifuko ya Saruji ikiwa ni mchango wake katika Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kaniha, Wilaya Biharamulo Mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad