Msajili Awapa Kongole CHADEMA Matumizi ya Tehama - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 17, 2021

Msajili Awapa Kongole CHADEMA Matumizi ya Tehama

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Ndg. Salum Mwalimu akifafanua jambo wakati wa zoezi la uhakiki wa namna chama hicho kinavyotekeleza matakwa ya sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi pamoja na kanuni zake mapema hivi karibuni. Kutoka kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. Peter Lyimo na Mkuu wa Kitengo cha Usajili wa Vyama vya Siasa, Bw. Muhidin Mapeyo.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. Peter Lyimo (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Usajili wa Vyama vya Siasa, Bw. Muhidin Mapeyo wakikagua orodha ya viongozi wa Chama cha Demkorasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar wakati wa zoezi la uhakiki lililofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu za chama hicho Zanzabar mapema hivi karibuni.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Elimu ya Uraia wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. Abuu Kimario na Afisa Sheria, Bi. Grace Mushi wakikagua nyaraka katika moja ya faili la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakti wa zoezi wa Uhakiki wa chama hicho katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu mjini Zanzibar mapema hivi karibuni.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Ndg. Salum Mwalimu akionyesha mpango kazi wa chama chake mbele ya watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (hawapo pichani) walipotembelea katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CHADEMA Zanzibar kwa ajili ya zoezi la uhakiki mapema hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Usajili wa Vyama vya Siasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), Bw. Muhidin Mapeyo akiangalia Kadi ya Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inayotolewa kwa njia ya Kidigitali walipokuwa katika zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya chama hicho mjini Zanzibar mapema hivi karibuni.Kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Elimu ya Uraia wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. Abuu Kimario, Afisa Sheria, Bi. Grace Mushi na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
 Ujumbe kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar mara baada ya kukamilisha zoezi la uhakiki katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CHADEMA Zanzibar mapema hivi karibuni.(Picha na ORPP) 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad