HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 15, 2021

Mfuko wa Maendeleo ya Filamu wa DW Akademie Kukuza Utengenezaji wa filamu kwa nchi za Kusini mwa Dunia

Kuanzia Septemba 14, 2021, watengenezaji wa filamu kutoka Tanzania na Uganda wanaalikwa kuomba fedha za kuwezesha uendelezaji wa matayarisho ya utengenezaji wa filamu na kupata mafunzo yatakayotolewa na DW Akademie.


Shirika la maendeleo ya habari la Ujerumani la DW Akademie, linalenga watengenezaji wa filamu kutoka Uganda na Tanzania ambao tayari wametengeneza filamu moja au zaidi, na wangependa kupata misaada katika utayarishaji wa miradi yao mipya ya filamu. Ifikapo Januari 2022 waombaji hadi watano, kutoka kila nchi hizi mbili, watachaguliwa na majopo tofauti ya majaji, ili kupokea ruzuku inayoweza kufikia Euro 10,000, pamoja na ushauri kwa kipindi cha mwaka mmoja, ili kuwasaidia kuendeleza ubora wa miradi yao ya filamu wanayotarajia kuifanya.

Programu hiyo itajumuisha warsha za kuongeza ujuzi katika filamu zitakazoendeshwa na wataalamu mbalimbali, hasa wanaotoka nchi za Kusini mwa Dunia. Mafunzo haya maalum yatawezesha washindi kuendeleza miradi yao kupitia hatua kadha za mwendelezo wa utayarishaji wa filamu. Mpango huo unafadhiliwa na Shirikisho la Ujerumani la Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (BMZ).

“Mfuko wa Maendeleo ya Filamu wa DW Akademie unakusudia kuwezesha kujulikana kwa filamu toka Uganda na Tanzania ndani ya nchi, kikanda na / au kimataifa. Tunataka kuhamasisha watengenezaji wa filamu ambao wanajitahidi kupaza sauti zao kwa kupitia hadithi wanazosimulia”, alisema Natascha Schwanke, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vyombo vya Habari, DW Akademie.

Mwito wa awali wa maombi kama haya uliotekelezwa nchini Ethiopia ulifana sana, na sasa tuna shauku kubwa ya kupokea maombi haya mapya.

“Watengenezaji wa filamu watano kutoka Ethiopia, nchi ya majaribio ya mfuko wa uendelezaji wa filamu, hivi sasa wanapokea msaada wa kifedha na mafunzo. Utayarishaji na uendelezaji wa miswada ya filamu ni awamu muhimu za uzalishaji wa filamu, ingawa fursa hizo  ni chache. Kwa kuzindua mfuko huo nchini Ethiopia, Tanzania na Uganda, DW Akademie inajitahidi kujenga mashirikiano na mitandao ya watengenezaji wa filamu katika kanda ya Afrika Mashariki. Ili kufanikisha lengo hili, DW Akademie inafanya kazi na washirika kadhaa wa kanda hii ambao ni pamoja na Maabara ya Filamu Zanzibar.

Martin Mhando, Mwenyekiti wa Maabara ya Filamu Zanzibar na Mkurugenzi Mtendaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF): amesema, “Kusema kweli hili ndio jibu kamili tunapoulizwa maana halisi ya maendeleo ya filamu: kujifunza kwa matendo na kutoka kwa wengine, jinsi ya kuifikisha hadithi kwenye kiwango bora zaidi kuliko ambavyo mtu mmoja pekee angeweza kufanya. Afrika imepata fursa ya kuzungumza na dunia kupitia hadithi ambazo zitadhihirisha jinsi ulimwengu ulivyo masikini zaidi kwa kukosa hadithi za Kiafrika, hekima ya Kiafrika, uzoefu wa Kiafrika”. 

Mfuko wa Maendeleo ya Filamu wa DW Akademie umeundwa mahsusi ili kusaidia watengenezaji wa filamu wanapokuwa katika hatua ya uendelezaji wa miradi yao ya filamu. Lengo kuu la mfuko huu ni kuimarisha tasnia ya filamu katika nchi za Kusini mwa Dunia,kwa waliochaguliwa, kupitia mkakati jumwuishi wa msaada wa kifedha na mafunzo.

Maelezo juu ya taratibu na maombi yanapatikana

hapa: akademie.dw.com/filmfund/

Maelezo juu ya programu ya ufadhili inayoendelea nchini Ethiopia inapatikana hapa: https://p.dw.com/p/3tP8e

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad