MAWAKILI , OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI WAPEWA MAFUNZO YA KISHERIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 29, 2021

MAWAKILI , OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI WAPEWA MAFUNZO YA KISHERIA

Mkurugenzi Mkuu wa Preston Legal Outsourcing Ltd (PLO) ambaye ni mshirika Mkuu (Mbia) wa kampuni ya Addleshaw Goddard (AG), Amani Tenga akifafanua jambo wakati wa Mafunzo ya kisheria waliyopewa na kampuni ya Addleshaw Goddard (AG) wakishirikiana na kampuni ya wazawa ya legal outsourcing; Preston Legal Outsourcing Ltd (PLO), mafunzo hayo yamehitimishwa leo katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam Septemba 29,2021.

KAMPUNI ya Kimataifa inayotoa huduma na Mafunzo ya kisheria, Addleshaw Goddard (AG) kwa kushirikiana kampuni ya wazawa ya legal outsourcing; Preston Legal Outsourcing Ltd (PLO) imetoa mafunzo ya kuongeza ujuzi kwenye kesi za Kimataifa na namna ya kuingia makubaliano ya mikataba ya Kisheria.

Mafuzo hayo ya siku mbili yaliyofadhiliwa na kampuni hiyo ya AG ya Dubai yenye makao yake Makuu nchini Uingereza na PLO yameendeshwa na wakurugenzi wa AG, Alex Sarac na Bevan Farmer. Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Mawakiliwa Serikali wa ofisi ya wakili Mkuu wa serikali.

Akiongea baada ya mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa PLO ambaye ni mshirika Mkuu (Mbia) wa kampuni hiyo ya Ag Amani Tenga amesema, mafunzo hayo yameenda vizuri na wanaimani mawakili wa serikali wameongeza ujuzi.
"Tunashukuru sana ushirikiano mkubwa tulipatiwa na ofisi nzuri ya Wakili Mkuu wa Serikali, na tunaamini mafunzo haya yatakuwa endelevu", amesema Tenga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kimataifa inayotoa huduma na Mafunzo ya kisheria, Addleshaw Goddard (AG), Bevan Farmer akizungumza wakati wa kufungua Mafunzo ya kisheria ya siku mbili (2) kwa mawakili wa Serikali kutoka ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali yaliyotolewa na kampuni ya Addleshaw Goddard (AG) wakishirikiana na kampuni ya wazawa ya legal outsourcing; Preston Legal Outsourcing Ltd (PLO), mafunzo hayo yamefanyika katika Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam yaliyoanza jana na kuhitimishwa leo Septemba 28,2021.
Mkurugenzi wa Idara ya Madai, Mussa Mbura akizungumza wakati wa Mafunzo ya kisheria waliyopewa na kampuni ya Addleshaw Goddard (AG) wakishirikiana na kampuni ya wazawa ya legal outsourcing; Preston Legal Outsourcing Ltd (PLO), mafunzo hayo yamehitimishwa leo katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam Septemba 29,2021.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri na Ubora, Mark mulwambo wa kwanza kulia akizungumza wakati wa Mafunzo ya kisheria waliyopewa na kampuni ya Addleshaw Goddard (AG) wakishirikiana na kampuni ya wazawa ya legal outsourcing; Preston Legal Outsourcing Ltd (PLO), mafunzo hayo yamehitimishwa leo katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam Septemba 29,2021. Katikati ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya usimamizi wa Mashauri na Ubora, Mercy Kyamba na Mkurugenzi wa Idara ya Madai, Mussa Mbura.
Mkurugenzi wa kampuni ya Addleshaw Goddard, Alex Sarac akizungumza wakati wa mafunzo ya kuongeza ujuzi kwenye kesi za Kimataifa na namna ya kuingia makubaliano ya mikataba ya Kisheria katika mafunzo yaliyohitimishwa leo Septemba 29, 2021 katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. kushoto ni Jay Kesaria kutoka kampuni ya Addleshaw Goddard ofisi ya Dubai.


Washiriki kutoka ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakifatilia mafunzo ya Kisheria yaliyomalizika leo Septemba 28,2021 jijini Dar es Salaam leo.


Wakurugenzi na mawakili kutoka ofisi ya wakili mkuu wa Serikali wakiwasili katika mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na kampuni ya Addleshaw Goddard (AG) kwa kushirikiana kampuni ya wazawa ya legal outsourcing; Preston Legal Outsourcing Ltd (PLO) jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad