BENKI YA NMB YAZINDUA AKAUNTI MPYA 'WEKEZA' ITAKAYOWAWEZESHA WATEJA KUWEKA AKIBA YA MUDA MREFU NA KUPATA RIBA KUBWA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 29, 2021

BENKI YA NMB YAZINDUA AKAUNTI MPYA 'WEKEZA' ITAKAYOWAWEZESHA WATEJA KUWEKA AKIBA YA MUDA MREFU NA KUPATA RIBA KUBWA


KATIKA kuwakumbusha wateja wao kuweka akiba ya maisha ya baadae, Benki ya NMB leo imezindua akaunti mpya inayoenda kwa jina la Wekeza itakayomuwezesha mteja kuweka akiba ya muda mrefu na kupata riba kubwa.

Hayo yamesemwa leo  na Afisa Mkuu wa Wateja na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi wakati akizindua akaunti hiyo ambapo amesema akaunti hiyo ya wekeza ni ya kwanza kuwahi kutokea nchini ambapo mteja atajitunzia fedha zake kuanzia Sh 250,000 na kupata riba kubwa mpaka 12 kulingana na miaka ambayo mteja anakusudia kuwekeza akiba yake.

Kupitia Wekeza mteja atakapojiandikisha kwenye akaunti hiyo atapata Bima ya Maisha bure na endapo atafariki au kupata ulemavu wa kudumu atalipwa mara Mbili ya akiba yake ambapo kima cha chini kupata bima hiyo ni Sh Milioni Mbili hadi Milioni 50.

Mponzi amesema muda wa kutunza akiba hiyo ni kati ya miaka sita mpaka 20 na riba hulipwa mara mbili kwa mwaka (Juni na Desemba) na Mteja atakuwa na uwezo wa kuongeza akiba kupitia matawi ya NMB, Mawakala wa NMB na NMB Mkononi.
 
" Hii maana yake ni kuwa, sisi kama benki iliyo salama zaidi nchini na kinara wa ubunifu katika utoaji wa huduma za benki, tunaendelea kuwekeza kimkakati kwenye teknolojia na mtandao wa matawi yetu  huku tukiimarisha uwezo wetu wa kuihudumia jamii. Lengo likiwa kuwawezesha wateja kuimarisha zaidi kipato na uchumi wao.

Tunabuni bidhaa zinazowasaidia wateja kuokoa muda na fedha na tunatumia teknolojia ya kisasa zaidi kufanya hivyo. Tunahitaji kila mtu kuzisimamia fedha zake akiwa na uelewa wa kutosha. Wateja watakao ruhusiwa ni wale wenye akaunti binafsi," Amesema Mponzi

Amesema lengo lao ni kupanua wigo wa akaunti zao binafsi ili kuwawezesha wateja wao kuwa na amani zaidi katika kusimamia fedha zao kwani akaunti hii ni kama kibubu chenye faida nyingi ambazo zitamsaidia mteja kuwa na tabia ya kujiwekea akiba kwa matumizi yenye malengo.
 
" Hili halijaja hivi hivi tu, benki ya NMB imeangalia soko la Tanzania taarifa za wateja wake na kuona kuwa watu wengi hawana tabia ya kuweka akiba kwa muda mrefu, hivyo kuna haja ya kuwaletea akaunti ambayo itawasaidia kuweka akiba," Amesema Mponzi.
 
Amesema huu ni muendelezo wa huduma ambazo NMB imekuwa ikianzisha ili kusaidia wateja wake kwa kutoa suluhisho la huduma za kibenki hapa nchini.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kulia), akizindua huduma mpya ya WEKEZA Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa NMB, Janet Rwegasila, Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalumu, Getrude Mallya.


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kulia), akizindua huduma mpya ya WEKEZA Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa NMB, Janet Rwegasila, Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalumu, Getrude Mallya.Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya WEKEZA Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa, Janet Rwegasila na Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad