HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 10, 2021

KESI YA TUHUMA ZA UGAIDI INAYOMKABILI MBOWE ,WENZAKE WATATU KUANZA KUSIKILIZWA SEPTEMBA 15 MWAKA HUU

 


KESI ya tuhuma ya  ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema)Freeman Mbowe na wenzake watatu inatarajia kuanza kusikilizwa Septemba 15, 2021 katika Mahakama Kuu kitengo cha makosa ya Uhujumu Uchumi  na Rushwa  maarufu kama Mahakama ya Mafisadi.

Hatua hiyo imekuja baada ya leoSeptemba 10, washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali.Katika kesi hiyo upande wa mashtaka unatarajiwa kuita mashahidi 24 na vielelezo 19  ili kuthibitisha  mashtaka dhidi  ya washtakiwa huku upande wa utetezi ukitarajiwa kuwa ma mashahidi 11.

Mapema akisoma maelezo ya awali,Wakili wa Serikali Tulumanywa Majigo amedai mshtakiwa wa kwanza, wapili na watatu wote walikuwa waajiriwa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), walioudhulia mafunzo ya ukomandoo katika kambi ya Ngerengere Mkoani Morogoro na waliofukuzwa kazi kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Majigo amedai kuwa washtakiwa hao watatu wanafahamiana huku mshitakiwa wa nne (Mbowe) akiwa  ni Mwenyekiti wa  Taifa wa chama cha siasa cha CHADEMA.

Wakili huyo amedai washitakiwa wote wanne wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kula njama, mshitakiwa wa kwanza na wapili wanashtakiwa na makosa ya kukutwa na mali iliyokusudiwa kutumika kutenda vitendo vya kigaidi huku mshitakiwa wa nne pekee  akikabiliwa na shitaka la kutoa fedha kwa ajili ya kufadhilii vitendo vya kigaidi.

 Majigo amedai Kwamba Julai mwama 2020 mbowe Aliomba Kukutana na Luten Denis Urio ambaye walikuwa wanafahamiana  awali.

 Waliafikiana kukutana na  baadae walikutana  katika moja  ya mgahawa uliopo maeneo ya mikocheni na wakiwa katika eneo hilo Mbowe alimuomba Luten amtafutie Makomando waliofukuzwa kazi ili wamsaidie  katika kutekeleza vitendo vya kigaidi ambavyo ni kulipua vituo vya mafuta mikusanyiko ya umma katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaama, Mwanza na Arusha.

Wakili ameendelea kudai kuwa Mbowe alimweleza Luteni Hurio lengo la kutaka kufanya hivyo ni kuleta taharuki kwa wananchi na kuharibu misingi iliyopo nchini kisiasa  na kiuchumi.

 Imeendelea kudaiwa kwamba, Mbowe alitoa Sh Laki 699,000 ili kuwezesha makomando aliotafutiwa ambao kwa sasa ni washtakiwa wenzake  kuja Dar es Salaam  ili kupanga namna ya kutekeleza ugaidi huo.

Inadaiwa kuwa Mbowe alikuwa akiwasiliana na wenzake kupitia mitandao ya Telegrama na kabla ya kukutekeleza kitendo hicho washtakiwa walikamatwa.

Ameeleza kuwa mshtakiwa  Adam Kusekwa  Mohamed Lingwenywa walikamatwa  eneo la Rau  wakiwa katika harakati za kumsababishia Sabaya majeraha na mshita pili alipopekuliwa alikutwa na siraha aina ya Pisto yenye Pastola tatu ambazo zilikuwa na nia ya kutumika katika vitendo hivyo.

Washitakiwa hao walisafirishwa hadi Dar es Salaam na walipohojiwa walikiri kujihusisha na vikao mbalimbali vya kigaidi na walimtaja mshtakiwa Khalfan Bwire na Mbowe kuwa sehemu ya wahalifu.

Agosti,9 mwaka 2020 mshitakiwa  Hassan Bwile , alikamatwa eneo la Changa'ombe na walipohojiwa katika kituo cha polisi Chang'ombe alikiri kuhusika katika kikao cha kutekeleza vitendo vya kigaidi.

Wakili amedai mshitakiwa Bwile alipopekuliwa katika makazi yake eneo la Yombo  alikutwa na mali za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  pamoja na kidaftari kidogo  na baada ya upekuzi fomu ya upekuzi ilidaiwa na kushikwa mshitakiwa

Amedai  kuwa kidaftari hicho kilipopelekwa katika maabara ya maandishi ilibainika kuwa mwandiko ulikuwa katika daftari hilo ni sawa na mwandiko wa mshitakiwa huyo.

Pia Agosti 11 mwaka 2020 Luteni Urio aliwasilisha simu yake aina ya Tecno katika maabara ya makosa ya mtandao kwa ajili ya uchunguzi na kuaminika kwamba meseji za mawasiliano  zilizokuja katika mtandao wa Telegram  kati Mbowe na Urio zilipatikana katika simu hiyo.

Amedai  Jeshi la Polisi liliendelea na  uchunguzi na Julai 20 mwaka huu Mbowe alikamatwa Mtaa wa Ghana ,Mwanza na kuunganishwa na washitakiwa wenzake ambao ni Bwire Kasekwa na Lingwenya

Baada ya kusomewa maelezo hayo, washitaliwa hao kupitia wakili wao Kibatala, mshtakiwa wa kwanza, wapili na watatu walikubali majina yao na anwani zao.

Pia washtakiwa hao wamekubali  walikuwa watumishi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kama Makomandona  na Ajira zao zilisitishwa kwa sababu ya vitendo vya utovu wa nidhamu.

Washitakiwa hao wamekiri kufanya kazi pamoja katika kikosi cha Jeshi Ngerengere  mkoa wa Morogoro  na kwamba wanafahamiana.

Kwa upande wa mshtakiwa  Freeman Mbowe), amekubaliana na majina na anwani yake ya makazi na kwamba ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema.Mbowe amekiri  kukamatwa Mtaa wa Ghana ,Iremela Mkoani Mwanza.

 Awali Wakili wa Utetezi Peter Kibatala alitaja kwa majina mashahidi saba pekee huku wengine wanne akiomba mahakama  kutoa kibali kwani  baadhi yao ni maafisa wa polisi na hivyo  wanaweza  kufikiwa kabla ya kutoa ushahidi  wao mahakamani hapo ombi ambalo limepingwa na upande wa Jamhuri.
 
 Hata hivyo, Jaji Siyani amesema, amesikiliza hoja za pande zote mbili amekubaliana na ombi la kibatala licha ya kuwa sheria hairuhusu ila inatoa mamlaka kwa mahakama kutoa uamuzi endapo kunakuwa na mazingira yanayolazimisha mashahidi kufichwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Spetembe15 kwa ajili ya Kuanza kusikiliza mashahidi wa upande wa Jamuhuri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad