Naibu
Katibu Mkuu wa CCM ( Bara) Ndugu Christina Mndeme akimnadi mgombea wa
ubunge jimbo la Ushetu kwa tiketi ya CCM Ndugu Emmanuel Cherehani
(kulia) kwenye viwanja vya Nyamilangano.Chama Cha Mapinduzi kimezindua
rasmi kampeni zake katika jimbo la Ushetu tarehe 26 Septemba 2021.(Picha
na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM ( Bara) Ndugu Christina Mndeme akimkabidhi Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 mgombea wa ubunge jimbo la Ushetu kwa
tiketi ya CCM Ndugu Emmanuel Cherehani (kulia) kwenye viwanja vya
Nyamilangano. Chama Cha Mapinduzi kimezindua rasmi kampeni zake katika jimbo la Ushetu terehe 26 Septemba 2021.(Picha na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu)
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndugu Christina Mndeme, leo
amezindua kampeni za ubunge jimbo la Ushetu wilayani Kahama mkoa wa
Shinyanga.
Mndeme,
amesema mgombea huyo Emanuel Peter Cherehani, anatosha kurithi viatu
vya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo ambaye pia alikuwa Waziri wa Ulinzi,
marehemu Elias Kwandikwa.
Uzinduzi
wa kampeni hizo umefanyika katika viwanja vya Nyamilangano, ambapo CCM
kimetumia fursa hiyo kumsimamisha Ndugu Emmanuel Peter Cherehani na
kumkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya 2020/2025 ya Chama hicho.
Katika
hatua hiyo, Mndeme alisisitiza kuwa Chererehani ana uzoefu wa uongozi
katika kutetea maslahi ya wananchi wa Ushetu, hususani katika masuala ya
kilimo, elimu, afya na maboresho ya miundombinu.
Aliongeza
kuwa, mgombea huyo amekuwa Mwenyekiti wa vyama mbalimbali vya ushirika
ikiwemo cha wakulima wa Tumbaku,Chama cha Mwadui na Ubangwa na mtetezi
wa maendeleo ya wakulima wa pamba.
Katika mkutano huo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali walihudhuria akiwemo Katibu wa Oganaizesheni wa CCM Ndugu Maudline Castiko, wabunge wa mkoa wa Shinyanga na mamia ya wananchi.

Sehemu
ya Watu waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za CCM katika jimbo la
Ushetu kwenye viwanja vya Nyamilangano. (Picha na CCM Makao Makuu)Sehemu
ya Watu waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za CCM katika jimbo la
Ushetu kwenye viwanja vya Nyamilangano. (Picha na CCM Makao Makuu)Naibu
Katibu Mkuu wa CCM ( Bara) Ndugu Christina Mndeme akiteta jambo na
mgombea wa ubunge jimbo la Ushetu kwa tiketi ya CCM Ndugu Emmanuel
Cherehani (kulia) kwenye viwanja vya Nyamilangano.Chama Cha
Mapinduzi kimezindua rasmi kampeni zake katika jimbo la Ushetu terehe 26
Septemba 2021.(Picha na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu)Naibu
Katibu Mkuu wa CCM ( Bara) Ndugu Christina Mndeme na mgombea wa ubunge
jimbo la Ushetu kwa tiketi ya CCM Ndugu Emmanuel Cherehani (kulia)
kwenye viwanja vya Nyamilangano wakiwapungia mkono wananchi
waliojitokeza kwenye ufunguzi wa kampeni.Chama Cha Mapinduzi kimezindua
rasmi kampeni zake katika jimbo la Ushetu terehe 26 Septemba 2021.(Picha
na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu)
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM ( Bara) Ndugu Christina Mndeme akihutubia wananchi
wa Ushetu ikiwa siku ya kwanza ya uzinduzi wa kampeni kwenye viwanja vya
Nyamilangano.Chama Cha Mapinduzi kimezindua rasmi kampeni zake
katika jimbo la Ushetu terehe 26 Septemba 2021.(Picha na Adam Mzee/ CCM
Makao Makuu)
Mgombea wa ubunge jimbo la Ushetu kwa tiketi ya CCM Ndugu Emmanuel Cherehani kwenye viwanja vya Nyamilangano.Chama
Cha Mapinduzi kimezindua rasmi kampeni zake katika jimbo la Ushetu
terehe 26 Septemba 2021.(Picha na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM ( Bara) Ndugu Christina Mndeme akiwaongoza
wanachama wa CCM na wananchi kucheza muziki wa Chama kutoka bendi ya TOT
kwenye viwanja vya Nyamilangano.Chama Cha Mapinduzi kimezindua rasmi
kampeni zake katika jimbo la Ushetu terehe 26 Septemba 2021.(Picha na
Adam Mzee/ CCM Makao Makuu)
No comments:
Post a Comment