RC KUNENGE AMUAGIZA MKANDARASI KUHARAKISHA UJENZI WA DARAJA LA MBUCHI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 12, 2021

RC KUNENGE AMUAGIZA MKANDARASI KUHARAKISHA UJENZI WA DARAJA LA MBUCHI

Na Mwamvua Mwinyi,Kibiti

MKUU wa Mkoa wa Pwani ,Abubakar Kunenge amemuagiza mkandarasi anayejenga  daraja la Mbuchi ,wilaya ya Kibiti kuharakisha ujenzi ili  kuwaondolea kero wananchi wanayoipata kwa sasa.

Kunenge aliyasema hayo ,alipokuwa kwenye ziara ya Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa huo ilipokuwa ikikagua miradi ya maendeleo likiwemo daraja hilo la Mbuchi

Kunenge alisema kukamilika kwa daraja hilo kutafungua njia kwa wakazi wa Vijiji vya Mbwela ambao wanasafirisha bidhaa kwenda Muhoro na maeneo mengine ya Wilaya ga Rufiji.

Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo ambayo inaondoa kero kwa wananchi.

Kaimu Mhandisi Mkazi wa Mradi huo Mtani Silasi alisema mradi huo utatekelezwa kwa miezi 12 na kwamba hadi kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi Bilion 6.1.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad