HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 24, 2021

Wizara ya Madini Kukusanya Bilioni 650

 

Mkurugenzi wa  Ukaguzi na Biashara ya Madini  kutoka Tume ya Madini Bw. Venance Kasiki akiwasilisha mada wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini leo Agosti 23, 2021 Jijini Dodoma.

Mwanasheria kutoka  Tume ya Madini Bi. Khadija Ramadhani akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini leo Agosti 23, 2021 Jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifutilia semina iliyolenga kuwajengea uwezo ili waweze kusimamia sekta ya madini na kushiriki katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya madini na Sheria ya Madini ya mwaka 2017.

 

Naibu Waziri wa Madini  Mhe.  Prof. Shukrani Manya (Mb) akieleza mikakati ya Wizara hiyo katika kuendelea kukuza sekta ya madini hapa nchini wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini leo Agosti 23, 2021 Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe.  Dastun  Kitandula (Mb) akizungumza wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini leo Agosti 23, 2021 Jijini Dodoma.

 

(Picha zote na MAELEZO)

******************************

Na Mwandishi wetu- Dodoma

Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya amesema Wizara hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa malengo ya kukusanya Bilioni 650 katika mwaka wa fedha 2021/22 yanafikiwa  kwa wakati kutokana na mikakati iliyowekwa.

Ameyasema hayo  leo  Agosti 23, 2021 Jijini Dodoma wakati wa Semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini inayolenga kuwajegea uwezo wajumbe hao ili waweze kutekeleza jukumu la Kuisimaia sekta hiyo kikamilifu.

“Tumejipanga kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwaa yanafikiwa na tunavuka kwa ushauri na maoni yatakayotolewa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini tunaamini kwa pamoja tutaweza kuongeza mchango wa  sekta ya madini na kukuza zaidi mchango wake katika kukuza uchumi”, alisisitiza Prof. Manya

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  ya Nishati na Madini Mhe. Dastun Kitandula amesema kuwa wajumbe wa Kamati hiyo wamejengewa uwezo na uwelewa kuhusu sheria ya Madini ya mwaka 2017, mfumo wa utoaji leseni za uchimbaji na utafiti wa madini na ushiriki wa watanzania katika sekta ya madini.

Akifafanua Mhe. Kitandula amesema kuwa wajumbe wa Kamati hiyo  wamepata uelewa wa kutosha kuhusu ushiriki watanzania   na faida wanazopata  kutokana na sekta ya madini kusimamiwa vizuri baada ya kufanyika kwa mageuzi makubwa yanayotoa fursa kwa watanzania kunufaika na rasilimali madini.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba  amesema kuwa pamoja na malengo mengine semina hiyo inalenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati hiyo ili waweze kuwasaidia katika kuelimisha wananchi katika maeneo yao na pia kuisimamia sekta hiyo .

Semina ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imefanyika Jijini Dodoma leo Agosti 23, 2021 na kushirikisha wabunge  ambao ni wajumbe wa Kamati hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad