HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 16, 2021

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DKT.NDUMBARO AAGIZA WATUMISHI WOTE WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUPITIA MAFUNZO YA KIJESHI

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amewataka Watumishi wote wanaofanya kazi katika Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wajiandae kisaikolojia kupitia mfumo wa mafunzo ya Kijeshi.

Ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi kilichopo Jijini Arusha ikiwa ni ziara ya kikazi Chuoni hapo ya kuwatembelea na kuzungumza na Watumishi hao ili kujua changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi

Amesema mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka ule wa kiraia kwenda katika mfumo wa Jeshi Usu, yanalenga kuleta suluhisho la kudumu katika kukabiliana na changamoto za usimamizi wa rasilimali misitu na nyuki pamoja na wanyamapori nchini.

Amesema hakuna Mtumishi yeyote wa Taasisi hizo atakayekwepa mafunzo hayo kwa vile hiyo ni sera ya Wizara huku akisisitiza kuwa hilo halikwepeki na yeyote ambaye hayupo tayari basi ahame wizara hiyo ndiyo itakuwa salimika yake

" Leo unaweza kuhamishwa kutoka Olmotonyi kwenda Shirika la Hifadhi za Taifa ( TANAPA) au TFS wenzako kule washakamilika tayari ni wanajeshi, wewe utakuwa raia" alihoji Dkt.Ndumbaro

Amesisitiza kuwa kila mtumishi aliyeko katika Taasisi hizo lazima apitie mafunzo hayo kwa sababu watakuwa wakihamishwa kutoka Taasisi moja hadi nyingine ndani ya Wizara hivyo endapo hajapitia mafunzo hayo itamuwia vigumu katika kutekeleza majukumu yao wakati akiwa raia katika mfumo wa kijeshi.

Amezitaja Taasisi hizo kuwa ni Mfuko wa Misitu Tanzania (TFF) Mfuko wa Wanyamapori Tanzania ( TWPF) Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB) Chuo cha Taifa cha Utalii ( NCT) Chuo cha Misitu Olmotonyi, Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi, Makumbusho ya Taifa (NMT), ChUo cha Nyuki Tabora (BTI), Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Taasisi ya Utafirti wa Misitu (TAFORI) TAWA, TANAPA na TFS

Kupitia agizo hilo,Dkt.Ndumbaro amezitaka Taasisi hizo kujiandaa kushiriki katika mafunzo hayo ambapo amesema mafunzo hayo yatatolewa kwa awamu awamu.

Akizungumza na Watumishi hao wa Chuo cha Olmotonyi, Dkt.Ndumbaro amesema anataka wanavyowafundisha wanafunzi wao ambao wataajiriwa TFS inayoendeshwa kijeshi ni lazima wakufunzi wao wawe wanajeshi kwanza

" Haiwezekani mnawafundisha Wanafunzi waende kuajiriwa huko TFS kama wanajeshi wakati ninyi sio wanajeshi, mnawafundisha nini " alihoji Ndumbaro

Awali, Kamishna Uhifadhi wa TFS, Prof.Dos Santos Silayo alieleza kuwa kwa vile TFS ndo imekuwa muajiri mkuu wa Wahitimu wa Chuo hicho hivyo wameanza utaratibu wa kuhakikisha baadhi ya kozi katika Chuo hicho ziwe na mafunzo ya kijeshi ili kuwaandaa wanafunzi wa Chuo hicho wanapoajiriwa na TFS

Alisema ili kuhakikisha hilo linafanikiwa wao kama TFS imekichagua Chuo hicho kuwa mojawapo ya kituo cha Mafunzo ya kijeshi kwa baadhi ya Maafisa kutoka TFS.


 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad