HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 6, 2021

GF TRUCKS & EQUIPMENT YAWAOMBA WATANZANIA KUTUMIA BIDHAA ZA NDANI KUKUZA UCHUMI

 

Kampuni ya  Gf Trucks & Equipment’s Ltd  ya jijini Dar es Salam imewaomba Watanzania hasa wadau wa sekta ya ujenzi na usafirishaji kupenda kununua bidhaa za ndani ili kusaidia kukuza uchumi.

Akizungumza  katika banda la Kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Sabasaba, Afisa Masoko wa GF Truck Juma Lukolo amesema, kama Watanzania watajenga utaratibu wa kununua bidhaa za ndani basi pia wataokoa fedha nyingi za kigeni.

Amesema Watanzania wamekuwa wakitumia fedha nyingi za kigeni na tena kwa gharama kubwa  kuagiza magari kutoka nje, hivyo kwa magari haya kutengenezwa humuhumu nchi kutaokoa muda, gharama na kusaidia kukuza uchumi wa ndani.

"Kwa sasa yale magari tuliyokuwa tukiagiza na kuyauza kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo sasa tunayatengeneza hapahapa nchini kwa lengo la kukuza uchumi, kutoa ajira kwa Watanzania huku tukikuza uchumi.

Kiwanda kinachotengeneza magari hayo cha GF Truck and Car Assemble ambacho kipo ndani ya majengo ya iliyokuwa Tamco.

Afisa Masoko wa GF Truck Juma Lukolo akizugumza

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad