HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 18, 2021

WANANCHI WAASWA KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI

 SEKTA mbalimbali, tawala za mikoa na serikali za mitaa, taasisi za umma, taasisi binafsi na mashirika ya kimataifa, na wananchi wote waaswa kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambayo ufanyika kila mwaka ifikapo Juni5.

Kwa mwaka huu 2021, Mgeni rasmi katika siku ya mazingira ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Juni 5 atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Isdori Mpango, maadhimisho yatakayofanyika jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 18, 2021 mkoani Dar es Salaam leo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo   amesema kuwa wadau wote wa mazingira waanze kuadhimisha siku hiyo mhimu kuanzia Juni Mosi hadi Juni 5, 2021 kwa kufanya shughuli mhimu za utunzaji wa mazingira.

"Nawaalika wadau wote wa mazingira kufanya shughuli zote mhimu kama vile kufanya usafi kwenye mazingira, kupanda miti kwenye maeneo ya makazi, kutumia nishati Mbadala wa mkaa, kutumia majiko majivu ili kuokoa miti inayoteketea kwa kutrngeneza mkaa."Amesema Jafo

Aidha Jafo amesema katika siku hizo za maadhimisho ya ya mazingira wananachi wataelekezwa jinsi sahihi ya utenganishaji wa aina mbalimbali za taka na kupewa elimu ya urahisisha uchakataji wa taka mbalimbali kwa kutengeneza bidhaa nyingine.

"Wananchi watahamasishwa kuwekeza katika utenganishi wa taka kabla hazijaenda kutupwa katika dampo, kwani taka taka nyingi huchanganywa kati ya zile taka za Pastiki na taka za kawaida." Amesema Jafo.

Licha ya hayo  Mei 29, 2021 Makamu wa Rais Dkt. Mpango ataongoza maandamano yatakayo hamasisha utunzaji wa mazingira, maandamano hayo yataanzia katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hafi eneo la Area D jijini Dodoma.

Amesema kuwa wahusika ma maandamano hayo ni wabunge, viongozi wote katika mamlaka za serikali za mitaa, madiwani, watumishi wa serikali, mawaziri, wananchi, wanafunzi pamoja na waandishi wa habari.

Waziri Jafo amesema kuwa wananchi watumie nishati mbadala ili kuokoa zaidi ya ekali milioni 48 zinazo haribiwa kwa ukatiji miti na kutengeneza mkaa kila mwaka. 

Kauli  mbiu ya kidunia kwa mwaka huu katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani ni Kuongoa mfumo Ikolojia na kauli mbiu kitaifa mwaka huu ni tutumie Nishati Mbadala kuongoa mfumo ikolojia.

 Hata hivyo amewaomba wanaikolojia kuleta teknolojia itakayoleta nishati mbadala itakayosaidia utunzaji wa mazingira na kuweka uwekezaji katika taka ili kutengeneza bidhaa nyingine.

Maandihisho haya ya siku ya mazingira yanakuja mara baada ya nchi za umoja wa mataifa kukaa pamoja na kujadiliana uharibifu unaofanywa katika mazingira uliokaliwa mwaka 1972 Na kuidhinisha siku ya Juni 5 kila mwaka kuwa siku ya mazingira duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad