Rais Samia ahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni Kampala nchini Uganda - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 12, 2021

Rais Samia ahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni Kampala nchini Uganda

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Kololo, kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni zilizofanyika katika uwanja huo uliopo Kampala nchini Uganda leo tarehe 12 Mei, 2021.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na kumpongeza  na Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya Sherehe za Uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Kololo Kampala nchini Uganda

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati Wimbo ya Taifa la Uganda ukipigwa mara baada ya Uapisho wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni uliofanyika katika Uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Marais wengine wa Nchi za Kiafrika pamoja na Wageni wengine waliohudhuria sherehe za Uapisho wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni zilizofanyika katika Uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda.


Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni akikagua Gwaride la Jeshi la Uganda huku akiwa kwenye Gari la wazi mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Uganda katika kipindi cha muhula mwingine katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika uwanja wa Kololo Kampala nchini Uganda katika sherehe za Uapisho wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni akizungumza mara baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda.  PICHA NA IKULU

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad