MAHAKAMA YA AFRIKA KUADHIMISHA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 21, 2021

MAHAKAMA YA AFRIKA KUADHIMISHA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA

Rais wa Mahakama ya Afrika ya watu na haki za binadamu Jaji Silvain Ore akizungumza na waandishi wa habari  mkoani Dar es Salaam leo Mei 21, 2021 kuhusu maadhimisho ya miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya watu na haki za binadamu. Kulia ni Afisa Habari wa mahakama ya ya Afrika ya watu na haki za binadam, Sukhdev Chhatbar.
Afisa Habari wa mahakama ya ya Afrika ya watu na haki za binadam, Sukhdev Chhatbar akifafanua jambo kuhusu kuweka majina ya Mwalimu Nyerere  na Rais wa Afrika Kusini kutumika katika mahakama na ukumbi wa mahakama ya Afrika. kushoto ni Rais wa Mahakama ya Afrika ya watu na haki za binadamu Jaji Silvain Ore
Afisa Itifaki wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu ( African Court on Human and Peoples Rights), Tamambele Simba akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dar es Salaam leo Mei 21, 2021.

KATIKA kuadhimisha miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu ( African Court on Human and Peoples Rights), mahakama hiyo imesema itawaenzi  viongozi wawili mashuhuri wa Afrika, mwasisi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Mwasisi wa Taifa la Afrika Kusini, Nelson Mandela kwa kuyatumia majina yao katika ukumbi wa mahakama hiyo na maktaba yake.

Rais wa Mahakama hiyo Jaji Silvain Ore ameyasema hayo leo Mei 21, 2020  jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya miaka 15 ya mahakama hiyo tangu kuanzishwa kwake yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Amesema, lengo kubwa na kufanya maadhimisho hayo ni kuelimisha jamii pamoja na kuifahamu mahakama hiyo ili waweze kujua shughuli zake na kuitumia.

"Katika maadhimisho hayo kutokuwepo na kongamano maalumu la majaji kutoka nchi mbali mbali za Afrika, mashindano ya wanafunzi na mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari wa nchi za Afrika.

Naye,  Afisa Habari wa mahakama hiyo, Sukhdev Chhatbar ameeleza kuwa jina la Mwalimu Nyerere litatumika katika jengo la Maktaba kubwa ya mahakama hiyo lililojaa vitabu mbali mbali vya sheria na haki za binadamu huku jina la Nelson Mandela likitumika katika ukumbi wa kusikiliza kesi wa Mahakama hiyo ambao kwa sasa unaitwa Kibo.

Akijibu swali la iwapo mahakama hiyo ina mpango wowote wa kuja kutumia lugha ya kiswahili katika kutoa maamuzi yake, Afisa Itifaki wa mahakama hiyo, Tamambele Simba amesema mahakama  kuwa Mahakama hiyo huendesha shughuli zake kwa kutumia lugha mbalimbali ikiwemo lugha ya Kiswahili.

Amesema, Kiswahili ni miongoni mwa lugha za Umoja wa Afrika (AU) na kwamba hata mahakamani hapo wanatumia lugha ya kiswahili.....mfano anapokuja mtu anayejua kiswahili basi kesi yake itaendeshwa kiswahili ama kwa kutumia mkalimani ama la."  Amesema Simba

“Mbali na kiswahili kule zinatumika pia lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kiswahili pia, Tunao wakalmani wazuri wa kutafsiri." Amesema Simba

 Mahakama ya kikanda iliyoanzishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kudumisha na kulinda haki za watu barani Afrika.

 Ilianzishwa kutokana na itifaki na mkataba wa Afrika wa watu na haki za Binadamu chini ya Ibara ya kwanza inayohusu  uanzishwaji wa Mahakama ya Afrika ya watu na haki za Bianadamu. 

Mkataba huo ilikubaliwa mwaka Juni 9,1998 na utekelezaji wake ukaanza Januari 25, 2004, lakini mahakama hiyo ilianza rasmi shughuili zake Novemba 2006.

Mpaka sasa ni nchi wanachama wa umoja wa Afrika (AU) 30 tu kati ya 55 ambazo zimesharidhia itifaki hiyo ikiwemo Tanzania.

Kati ya nchi hizo ambazo zimesharidhia itifaki hiyo ni nchi hadi kufikia Juni 2019 ni nchi tisa tu ndizo zilikuwa zimeshatoa tamko, la kuridhia itifaki hiyo ikiwemo Tanzania, hatua ambayo huwawezesha mtu binafsi na asasi zisizo za kiraia (NGO) kufungua kesi katika mahakama  hiyo kabla ya Tanzania kujitoa katika hatua hiyo  mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad