IGP SIRRO AZUNGUMZIA AGIZO LA RAIS SAMIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 8, 2021

IGP SIRRO AZUNGUMZIA AGIZO LA RAIS SAMIA

 

 

Kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza na Wazee wa jiji la Dar es salaam, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo huku akiwaagiza Wenyeviti wa serikali za Mitaa kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi vitakavyosaidia kukomesha vitendo ya kihalifu.

 IGP Sirro amesema hayo leo wakati akiongea na maofisa wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam huku akiwapa mwezi mmoja makamanda hao kuhakikisha wanakomesha vitendo vya uhalifu katika jiji hilo.

Aidha, IGP Sirro ameendelea kusisitiza hasa kwa watu wanaopata msamaha wa vifungo kutoka gerezani kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani ambapo amesema Jeshi la Polisi litaendelea kutumia sheria zilizopo ili kuwashughulikia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad