NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI MWITA WAITARA AKUTANA NA MENEJIMENTI ZA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA YAKE JIJINI DAR - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 25, 2021

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI MWITA WAITARA AKUTANA NA MENEJIMENTI ZA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA YAKE JIJINI DAR

KATIKA Kuimarisha utendaji kazi na kuleta tija kwa jamii na Serikali Naibu Waziri na Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara  amekutana na Menejimenti za Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo Mkoani Dar es Salaam na kujadili ubireshaji wa Wizara hiyo.

Katika kikao hicho,  Waitara amepata nafasi ya kupokea taarifa mbalimbali za utekelezaji kutoka katika Taasisi hizo.

Aidha, Waziri Waitara amezitaka taasisi hizo kufanya kazi kwa weledi na ubunifu ili kuiwezesha Serikali kupata mapato ambayo yatasaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.

 Aidha ameahidi kutembelea kila taasisi ili kujadiliana kwa kina juu ya utekelezwaji wa   majukumu, changamoto, mafanikio na mikakati ya kusonga mbele katika kutekeleza majukumu ya wizara.

Vilevile Waitara amezitaka menejimenti zote kuipitia upya hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipolihutubia Bunge na watanzania wote Aprili 22, 2021 ili kuyachambua maono ya Mhe. Rais na kujipanga vizuri kuyatekeleza.

Mkutano wa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara na menejimenti za Taasisi ni mkutano wa kwanza tangu Mhe. Waitara alipoteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad