HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 12, 2021

WALIOIBA DAWA ZA MILIONI 13.5 SONGWE KUCHUKULIWA HATUA

 


Na. Catherine Sungura, Songwe

Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima  amewataka watumishi wa Afya wa Mkoa wa Songwe walioiba dawa za shilingi milioni 13.5 na kurudisha milioni 10.6 wafikishwe Kwenye vyombo vyote vya Sheria ikiwemo Polisi, PCCB na  kisha Mahakamani kwa kadri ya makosa ya kila mmoja.

Dkt.Gwajima ameyasema hayo leo Mara baada ya kusomewa ripoti ya Mkoa na Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Hamadi Nyembea wakati ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa pamoja na kuangalia Hali ya utoaji wa huduma za afya mkoani hapa.

Amesema wapo baadhi ya watumishi katika sekta hiyo ambao sio waadirifu na hivyo wameshindwa kuheshimu Mali ya Umma na kusababisha hasara kubwa ya bidhaa za Dawa nchini.

Dkt.Gwajima aliongeza kuwa kulipwa kwa baadhi ya fedha hizo ni dhahiri kwamba upo udokozi wa dawa na endapo ukaguzi wa dawa ulofanywa na Mkoa ingefanyika na nje ya halmashauri kungeweza kuwa na hesabu kubwa ya upotevu wa bidhaa za dawa.

"Sasa natangaza Vita ya wadokozi wa bidhaa za afya na Vyombo vyote vya kisheria sasa vitahusika na vita dhidi ya wabadhirifu wa bidhaa za dawa Mana wapo watumishi wachache wanarudisha nyuma ugavi wa bidhaa za Dawa na kushindwa kusimamia vyema Mali ya Serikali.

Hata hivyo aliagiza watumishi hao baada ya kuchukuliwa hatua za kisheria,wafikishwe Kwenye Bodi na Mabaraza ya kitaaluma ili wachukuliwe hatua kulingana na Mabaraza hayo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela amesema amepokea maagizo hayo na kuagiza vyombo vya kisheria mkoani hapo kuanza kazi Mara moja.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad