HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 10, 2021

Serikali kuanzisha vituo vya kuhakiki ubora wa bidhaa kabla ya kuzipeleka nje

Naibu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE), Dkt. Emmanuel Munisi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (Machi 10, 2020) wakati wa akifungua mkutano wa wadau wa biashara kutoka sekta mbalimbali nchini ulioandaliwa na Mradi wa kuwasaidia Wakulima kuongeza thamani ya mazao na namna ya kufikia Masoko (MURKUP).

SERIKALI imepanga kuanzisha vituo vitakavyofanya kazi ya kuhakiki ubora wa bidhaa za wafanyabiashara kabla ya kupeleka nje ya nchi ili kujua kama zina na ubora wa kimataiafa ama la.

Naibu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE), Dkt. Emmanuel Munisi akimuwakilisha Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara, ameyasema hayo leo Machi 10, 2021wakati akifungua mkutano wa wadau wa biashara kutoka sekta mbalimbali nchini ulioandaliwa na Mradi wa kuwasaidia Wakulima kuongeza thamani ya mazao na namna ya kufikia Masoko (MURKUP).

amesema, kukosekana kwa vituo vya kuhakiki bidhaa nchini imekuwa ikichangia kurudisha nyuma uendeshaji wa biashara hizo kwani wafanyabiashara wamekuwa wakipoteza muda sana katika kuuza bidhaa zao kwa kulazimika kupeleka bidhaa hizo nje ya nchi ili kuzihakiki kabla ya kuziingiza sokoni kuuza.

Dk.Munisi amesema vituo hivyo vikianzishwa, vitasaidia kufanya uhakiki na kuwapunguzia usumbufu wafanyabiashara kusafiri kwenda nje kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo kwani kitendo cha wafanyabiashara kwenda kuhakiki bidhaa zao nje ya nchi kwa ajili ya kujua kama zina ubora wa kimataifa kinawachelewesha na kuwachukulia muda mwingi wao kufanya biashara zao.

“Vituo hivyo tunavianzisha na kesho tutafungua chama kimojawapo cha kuhakiki ubora huo wa bidhaa za kwenda nje ya nchi na kabla ya kuingia nchini.”

Aidha dk. Munisi amesema Serikali imefanya jitihada mbalimbali za kuondoa vikwazo katika biashara ikiwamo tozo mbalimbali ambapo Markup katika tafiti zake walizofanya kuanzia mwaka 2013 na mwingine wa hivi karibuni walibaini kuwa vipo vikwazo vya biashara ambavyo ni zaidi ya kodi vinavyowekwa ikiwamo sheria, kanuni na taratibu ambazo wanasema zinarudisha biashara nyuma ndani ya Afrika Mashariki, SADC na Ulaya.

"Sisi kama serikali tumelichukua hilo na kulifanyia kazi, na tunafahamu wafanyabiashara wote wanatoka katika sekta binafsi ambayo ndiyo injini ya maendeleo na uchumi wa nchi na Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na taasisi mbalimbali hivyo tayari tumeondoa tozo 170 ambazo zilikuwa zinachangia wafanyabiashara kushindwa kuingiza na kupeleka bidhaa nje ya nchi,”amesema Dk.Munisi.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa kuwasaidia Wakulima kuongeza thamani ya mazao na namna ya kufikia Masoko(MURKUP) Safari Fungo amesema katika utafiti huo ambao umefanywa na wafanyabiashara hao, wamebaini changamoto mbalimbali ambazo wafanyabiashara wanakutana nazo katika uingizaji na upelekaji wa bidhaa nje ya nchi.

"Katika utafiti huo asilimia 50 ya changamoto zilizopo kwenye biashara zipo kwa wafanyabiashara kushindwa kukidhi mahitaji ya soko ya ubora na viwango kwenye masoko ya nje .

Amesema kikwazo kingine ni uwapo wa sheria, kanuni na taratibu zisizoendana na uendeshaji wa biashara hiyo hususan katika eneo la uendeshaji za kutoa nje kuingiza nchini na zile za kupeleka nje ya nchi.

Fungo amesema wafanyabiashara wanahitaji kupata idhibati ili kuonesha umahiri kama dhaa zao zimepimwa na namna gani zimekidhi vigezo, ambapo katika kipengele hiki bado ni changamoto.

ratibu wa Mradi wa kuwasaidia Wakulima kuongeza thamani ya mazao na namna ya kufikia Masoko(MURKUP) Safari Fungo akizungumza mara baada kufunguliwa mkutano wa wadau wa biashara kutoka sekta mbalimbali nchini ulioandaliwa na Mradi wa kuwasaidia Wakulima kuongeza thamani ya mazao na namna ya kufikia Masoko (MURKUP).
Watoa maada wakiwa katika akifungua mkutano wa wadau wa biashara kutoka sekta mbalimbali nchini ulioandaliwa na Mradi wa kuwasaidia Wakulima kuongeza thamani ya mazao na namna ya kufikia Masoko (MURKUP).
Baadhi ya wachangiaji katika akifungua mkutano wa wadau wa biashara kutoka sekta mbalimbali nchini ulioandaliwa na Mradi wa kuwasaidia Wakulima kuongeza thamani ya mazao na namna ya kufikia Masoko (MURKUP).
Baadhi ya washiriki wa akifungua mkutano wa wadau wa biashara kutoka sekta mbalimbali nchini ulioandaliwa na Mradi wa kuwasaidia Wakulima kuongeza thamani ya mazao na namna ya kufikia Masoko (MURKUP), wakisikiliza maada zinazoendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad