HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 8, 2021

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MARIAM MWINYI AMEZINDUA MRADI WA AMKA MWANANGU SOMA KWA BIDII

 

 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimsikiliza mmoja wa shuhuda wa matumizi ya Dawa za Kulevya Ndg. Suleiman Said Humoud akitowa maelezo wakati wa uzinduzi wa Mradii wa Jumuiya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, uliozinduliwa katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar na (kushoto kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na (kulia kwake) Mwenyekiti wa Taasisi ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) Mhe. Tauhida Cassian Gallos.(Picha na Ikulu)
 
BAADHI ya Wabunge na Viongozi wa mbalimba na Wananchi wakifuatilia Uzinduzi wa Mradi wa Amka  Mwanangu Soma kwa Bidii, wakati Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuuzindua Mradi huo jana usiku 7-3-2021, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii wa Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) na Mshika Fedha wa Taasisi hiyo Bi, Valeria Rashid Haroub, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar jana usiku 7-3-2021.(Picha na Ikulu)
 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii Ili Kutengeneze Kesho Yako, hafla hiyo imefanyika jana usiku 7-3-2021, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Risala ya Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) na Katibu wa Jumuiya hiyo Bi. Tatu Hussein Abdalla, wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar jana usiku 7-3-2021.(Picha na Ikulu)
 
BAADHI ya Mawaziri na Viongozi wa Taasisi za Serikali wakimsiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, akihutubia katika hafla hiyo ya Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii Ili Kutengeneza Kesho Yako, uzinduzi huo umefanyika jana usiku 7-3-2021 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimtunza msanii wa Kikundi cha Zanzibar One, wakati wakitowa burudani katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) Amka Mwanangu Soma kwa Bidii Ili Kutengeneza Kesho Yako, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akionesha Tunzo aliyokabidhiwa na Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar ( RAWWAZA) ya  ‘Kumpongeza Mama Mariam Mwinyi Kwa Kuungana Nasi Zidi ya Kuwapigania Wanawake na Watoto Zanzibar’ baada ya kukabidhiwa na Walezi wa Jumuiya hiyo Mhe. Taufik Salim Turky na Mhe Faharia Khamis Shomar. Wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii Ili Kutengeneza Kesho Yako.(Picha na Ikulu)
 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Jahazi iliotolewa na Jumuiya ya RAWWAZA kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, akikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii Ili Kutengeneza Kesho Yako, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwariam Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, waliosimama nyumba na waliokaa kutoka (kushoto kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A”Unguja Bi. Suzan Kunambi na (kulia kwake) Mwenyekiti wa RAWWAZA Mhe. Tauhida Cassian Gallos, baada ya kumalizika kwa hafla ua Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma Kwa Bidii uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwasalimia na kuwaaga wageni waalikwa katika hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, baada ya kuuzindua Mradi huo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanziba.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad