KAMPUNI YA ELVOMI YASHIRIKI MAONESHO YA WANAWAKE DAR, YAWAASA WANANCHI KUTUMIA VIPODOZI VYENYE UBORA KWA AFYA YA NGOZI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 4, 2021

KAMPUNI YA ELVOMI YASHIRIKI MAONESHO YA WANAWAKE DAR, YAWAASA WANANCHI KUTUMIA VIPODOZI VYENYE UBORA KWA AFYA YA NGOZI

Baadhi ya bidhaa za Elvomi zilizo katika Maonesho ya Viwanda ya  Wanawake Tanzania yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama Dar es Salaam.
Afisa Mauzo Msaidizi kutoka kampuni ya Elvomi, Suzan Winnes akizungumza na mteja katika Maonesho ya Viwanda ya  Wanawake Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama Mkoani Dar es Salaam leo.
Bidhaa ya Sabuni ya Nazi.
Baadhi ya bidhaa za Elvomi zilizo katika Maonesho ya Viwanda ya  Wanawake Tanzania yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama Dar es Salaam.
Afisa Mauzo Msaidizi kutoka kampuni ya Elvomi, Suzan Winnes akitoa maelezo juu ya ubora wa sabuni ya kunawia mikono katika Maonesho ya Viwanda ya  Wanawake Tanzania yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Posta Dar es Salaam.
Afisa Mauzo Msaidizi kutoka kampuni ya Elvomi, Suzan Winnes akitoa maelezo juu ya Ubora wa Sabuni ya Nazi ya Kipande katika maonesho yanayofanyika katika Viwanja vya Posta Mkoani Dar es Salaam.
Afisa Mauzo Msaidizi kutoka kampuni ya Elvomi, Suzan Winnes akiwa na Mafuta ya Nazi ya Mgano.

KAMPUNI ya Elvomi inayojishughulisha na utengenezaji pamoja na usambazaji wa bidhaa za vipodozi asilia hapa nchini yawaasa wananchi kutumia bidhaa zenye ubora ili kila mmoja apendeze kulingana na rangi yake.

Akizungumza na Michuzi blog katika viwanja vya Posta Kijitonyama mkoa wa Dar es Salaam wakati wa Maonesho ya Viwanda ya  Wanawake Tanzania, Afisa Mauzo Msaidizi kutoka kampuni ya Elvomi, Suzan Winnes amesema kuwa katika meza yao wanauza Sabuni ya kipande na maji, Mafuta ya Nazi ya Maji na Mgando ambayo ni bora zaidi katika ngozi ya kila mtu.

Amesema kuwa Ubora wa mafuta ya Elvomi ya nazi nimazuri kupaka kwenye nywele kwasabubu mafuta hayo yanayayuka kwa urahisi pia mafuta hayo ni mazuri kwa kupaka kwenye kila aina ya ngozi na kukuacha ukiwa na rangi halisi.

Suzan akizungumzia upande wa sabuni amesema kuwa sabuni zinazotengenezwa na Kampuni ya Elvomi nazo ni za nazi na zinafaida kemu kemu kweny ngozi kwani zinauwezo wa kuondoa vipele vya joto na chunusi na kufanya ngozi kuwa laini kwa sabuni za kunawia mikono zinaacha mikono ikiwa laini na yenye nyevunyevu isiyosababisha mikono kubabuka.

Kama ukitaka maelekezo ya Bidhaa za Elvomi wasiliana nao namba ya simu +255769223388 Instagram: @elvomi__ na Email:elvomicompany@gmail.com

Amesema Katika kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka kampuni ya Elvomi nayo imeshiriki katika Maonesho ya Viwanda ya  Wanawake Tanzania ikiwa njia mojawapo ya kutangaza na kujifunza biashara mbalimbali ambazo wanawake wanazifanya katika jamii.

Maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya posta kijitonyama Mkoani Dar es Salaam yalizinduliwa naa Naibu Waziri Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe ikiwa ni chachu kwa wanawake kujiinua kiuchumi.

Maonesho yanaendelea kufanyika katika viwanja hivyo yakiwa na kaulimbiu isemayo 'MWANAMKE NA UWEKEZAJI WENYE TIJA KWA VIWANDA ENDEVU' yanataraiwa kufikia kilele chake Machi 8, 2021 kwenye kilele sha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad