HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 4, 2021

Airtel na TPB Bank waungana kupata suluhisho huduma za Fedha kidigitali Nchini

 

 Airtel Tanzani imetangaza kuiingia ubia na Benki ya TPB kwa lengo na dhamira ya kuboresha na kupanua wigo wa huduma za kifedha nchni Tanzania, Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money imekua ikitoa huduma mbalimbali za kifedha kwa njia ya mtandao ikiwemo kutoa na kupokea pesa popote, kulipia Ankara mbalimbali kama vile LUKU, DSTV, malipo mbalimbali ya serikali, huduma za Maji kama Dawasco na nyingine nyingi .

Akiongea wakati wa Mkutano maalum na waandishi wa habari wakutangaza Ubia kati ya Airtel na TPB benki, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema “Ubia tunaoingia hapa leo utasaidia sana kuboresha huduma tunazotoa kwa kuwafaidisha zaidi mawakala wetu wa Airtel Money waliopo kila mahali nchini ambapo benki ya TPB imefika. 

Pia Wateja wa Airtel Money sasa watakuwa na uhakika kufanya miamala yao kwa uhakika kabisa wakiwa popote kama vile kuhifadhi au kutoa pesa toka benki ya TPB kwenda moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money ili kufanya malipo mbalimbali ya huduma kama vile LUKU, Ankara za Maji, DSTV, au kukamilisha malipo mbalimbali ya tozo za serikali.


Nchunda alielezea kuwa “Mawakala sasa hawana haja ya kubeba bulungutu la fedha na kusafiri umbali mkubwa kupata salio au (Float), sasa watahudumiwa kwenye tawi lolote la TPB karibu yake, Hii itasaidia sana kwenye kuokoa muda na fedha ambazo walizitumia kama nauli kwenda umbali mrefu ili kupata salio/Float, sasa ni haraka zaidi na salama. Ubia wetu na Benki ya TPB unalengo la kuendeleza ubunifu katika utoaji wa huduma za fedha kiditali kwa kupunguza madhara yanayowakumba mawakala au wateja wetu wanaposafiri umbali mrefu kufata huduma, sasa watajiunga na benki ya TPB karibu yao na kufanya miamala yote kigitali kupitia Airtel Money kwenda benki au kutoka benki kwenda Artel Money. 

Muunganiko wetu utaendelea kukamilisha dhamira yetu tuliyojiwekea sisi wabia ya kutoa huduma nafuu, kwa haraka, bila mipaka ili kikidhi mahitaji ya wateja wetu ya kila siku alisisitiza Nchunda Akiongea kwa niaba ya TPB benki Mkurugezi wa huduma za kimtandao Bw, Jema Msuya alisema “TPB tunaaamini suluhisho la huduma za kifedha katika utoaji huduma unatija sana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi, hivyo basi Ubia wetu na Airtel ni muendelezo wa kuendelea kupunguza changamomoto za pande zote yaani za wale waliofikiwa na huduma za kibenki na ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki popote walipo kwa kuwa sasa watapata huduma kwa njia ya mtandao na kufanya malipo kidigitali. 


“Benki ya TPB kila tuponakuja na huduma yenye ubunifu zaidi lengo letu ni kuongeza au kutoa suluhisho zaidi kwa wateja wetu pamoja na kuwapatia huduma kwa unafuu huku tukizingatia ubora zaidi. Ubia wetu na Airtel Money leo hii unadhihirisha dhamira yetu hiyo ya kutoa huduma kabambe, zenye usalama bila kuzingatia mipaka yaani huduma popote ulipo. Kila mteja wetu anaweza kujipatia huduma zetu akiwa na simu yake kiganjani kutokana na ubia huu sasa.” Alisema bw, Msuya .


Ili wakala wetu au Mteja aweze kupata huduma hii ya atatakiwa kutembeleia tawi letu la TPB bank na kujaza fomu maalum ya huduma bila kupoteza wakati ataanza kufurahia huduma zetu kwa kupiga *150*60# cahagua namba 0 Ongeza Pesa
Select 2 Hamisha toka Benki
Select 4 TPB Benki na ufuate Maelekezo.

Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda (kulia) na Mkurugezi wa huduma za kimtandao Jema Msuya kutokaTPB benki wakionyesha bango baada ya kuzindua ubia baina ya Airtel ba Benki ya TPB ambapo Wateja wa Airtel Money sasa watakuwa na uhakika kufanya miamala yao kwa uhakika  wakiwa popote kama vile kuhifadhi au kutoa pesa toka benki ya TPB kwenda moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money ili kufanya malipo mbalimbali ya huduma kama vile LUKU, Ankara za Maji, DSTV, au kukamilisha malipo mbalimbali ya tozo za serikali.


Mkurugezi wa huduma za kimtandao Jema Msuya kutokaTPB benki akiongea jijini Dar es Salaam wakati akitangaza ubia baina ya Airtel ba Benki ya TPB ambapo Wateja wa Airtel Money sasa watakuwa na uhakika kufanya miamala yao kwa uhakika  wakiwa popote kama vile kuhifadhi au kutoa pesa toka benki ya TPB kwenda moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money ili kufanya malipo mbalimbali ya huduma kama vile LUKU, Ankara za Maji, DSTV, au kukamilisha malipo mbalimbali ya tozo za serikali. Kulia ni Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda



Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda akiongea jijini Dar es Salaam wakati akitangaza ubia baina ya Airtel ba Benki ya TPB ambapo Wateja wa Airtel Money sasa watakuwa na uhakika kufanya miamala yao kwa uhakika  wakiwa popote kama vile kuhifadhi au kutoa pesa toka benki ya TPB kwenda moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money ili kufanya malipo mbalimbali ya huduma kama vile LUKU, Ankara za Maji, DSTV, au kukamilisha malipo mbalimbali ya tozo za serikali. Kushoto ni Mkurugezi wa huduma za kimtandao Jema Msuya kutokaTPB benki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad