
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Anna Mghwira
akiangalia viatu wakati akitembelea banda la International Leather
Industries Co. Ltd) lililopo Katika maonesho ya nne ya programu ya
uwezeshaji kiuchumi wananchi yanayofanyika Katika viwanja vya kumbukumbu
ya Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.
Na Woinde Shizza Michuzi Tv - ARUSHA
WATANZANIA
wametakiwa kupenda na kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini zikiwemo
bidhaa za ngozi zinazozalishwa na kiwanda cha Kilimanjaro kinachozalisha
bidhaa zenye ubora wa kimataifa .
Hayo
yamebainishwa na Fredrick Njoka ambaye ni Afisa uhusiano na Meneja
Masoko wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro (Kilimanjaro
International Leather Industries Co. Ltd) wakati wa maonesho ya nne ya
mifuko ya baraza la uwezeshwaji kiuchumi na kueleza kuwa kiwanda hicho
kinamilikiwa kwa ubia kati ya PSSSF na Jeshi la Magereza.
Njoka
amesema, Watanzania wanatakiwa kujua kuwa kauli mbiu ya Tanzania ya
viwanda ni pamoja na kupenda na kuunga mkono vitu na bidhaa
zinazotengenezwa na viwanda vya Tanzania na kuhamasishana watanzania
wenyewe kwa wenyewe kupenda vitu vya ndani.
Amesema
kuwa kiwanda hicho kimesaidia upatikana kwa soko la uhakika la ngozi
ghafi kutoka kwa wafugaji, Kuongeza thamani ya ngozi inayozalishwa hapa
nchini kutokana na mpango wa mafunzo maalumu kwa wafugaji na ajira za
moja kwa moja 3000 na zaidi ya ajira 7000 zisizo za moja kwa moja katika
mnyororo wa thamani na huduma.
Amesema kiwanda hichi kinasaidia kuongeza mapato kwa Taifa kupitia kodi mbalimbali.
"Pia
kiwanda hiki kina manufaa makubwa kwa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na
mikoa jirani kwa kuboresha mfumo wa maisha na kuongeza kipato kwa
wakazi, majengo na miundombinu na kinaokoa fedha za kigeni kwa kupunguza
uingizaji wa bidhaa za ngozi nchini na kuongeza mapato ya fedha za
kigeni kwa kuuza bidhaa za ngozi nje ya nchi.'' Amesema.
No comments:
Post a Comment